Ads

RUWASA YA MTUA MAMA NDOO KICHWANI.

 


Na wellu Mtani

AKUANZISHWA kwa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira ni sehemu ya ukombozi wa watanzania pamoja na utekelezaji wa kaulimbiu ya kumtua mama ndoo kichwani

Hali hiyo inatokana na na ukweli kwamba kutokana na kuwanzishwa kwa Ruwasa imeonesha matumaini makubwa kwa wananchi katika suala zima la upatikanaji wa maji kwa asilimia kubwa tofauti na hapo awali.

Aidha kuwanzisha kwa Wakala huyo imetajwa kuwa ni matokeo ya mabadiliko makubwa yaliofanywa na Serikali ili huduma ya maji vijijini kuongezeka, kubureshwa na kuwa endelevu.

Akiongea na waandishi wa habari sambamba na kutoa maelezo kwa mkuu wa Wilaya ya Singida Dk.Paskas Mragili,alipotemvelea katika banda hilo kwenye maonesho ya nane nane katika viwanja vya nzuguni jijini Mhandisi Mwajuma Kondo amesema  kuwa malengo ya RUWASA kwa muda mfupi ni kusimamia ujenzi wa miradi ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa Mazingira Vijijini yanafikiwa malengo ya asilimia 85 ifikapo Desemba 2023.

Amesema Mipango hiyo inahusisha na Kuendeleza ujenzi wa miradi 23 iliyo Katika hatua mbalimbali za utekekezaji kupitia fedha za mfuko wa Taifa wa maji (NWIF) na Bajeti ya mfuko Mkuu wa Serikali.

Aidha amesema lengo lingine la kuanzishwa kwa Ruwasa ni kuendelea utekekezaji wa mpango wa malipo (payment by results) ambapo katika mpango huo Kuna jumla ya miradi 50.

"Baadhi ya miradi inakarabatiwa na kupanuliwa na miradi mingine mipya iliyojengwa huku miradi 73 inaendelea kukamilika itaongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 794 ya sasa na kufikia asilimia 87.3 . 

No comments