Ads

BREAKING NEWS :RUTO ASHINDA URAIS KENYA ,MWENYEKITI MWENZA WA TUME AJITOA DAKIKA ZA MWISHO.




Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imemtangaza  William Ruto  kuwa mshindi (Rais Mteule) wa Uchaguzi uliofanyika Agosti 9 mwaka huu, kwa kupata kura  - 7,176,141 (50.49% ,kwa ushindi huu Ruto anakuwa  Rais wa Tano wa Kenya. 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya Juliana Cherera amesema “Hatuwezi kuwa sehemu ya matokeo ambayo yanaenda kutangazwa katika Bomas of Kenya, kwa sababu ya hali ya kutoeleweka ya awamu hii ya mwisho.

Muungano wa Azimio la Umoja unadai kuwa mfumo wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya IEBC ulidukuliwa.

Akizungumza na vyombo vya habari kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya urais, wakala Mkuu wa Raila Odinga, Saitabao Ole Kanchory alisema ndiyo sababu alisema Bomas ni 'eneo la uhalifu'.

"Tuna ripoti za kijasusi kuwa mfumo wao ulipenya na kudukuliwa na kwamba baadhi ya maafisa wa IEBC walifanya makosa ya uchaguzi na baadhi yao walipaswa kukamatwa," alisema.

Kanchory alisema IEBC inafaa kuwajibika kwa Wakenya akiongeza kuwa hawajaweza kuthibitisha matokeo ya uchaguzi wa urais.

Mchanganuo wa kura  walizo pata wapinzani wa Ruto.

William Ruto - 7,176,141 (50.49%)

Raila Odinga - 6,942,930 (48.85%)

George Wajackoyah - 61,969 (0.44%)

Waihika Mwaure - 31,987 (0.23%)

No comments