Ads

PADRE HAIMIZA MASOMO YA DINI MASHULENI KUPEWA KIPAUMBELE .

 



Na Wellu Mtaki,Dodoma

PADRE wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makole Jimbo kuu la Dodoma Gaitan Maswenya ametaka viongozi wenzake wa madhehebu ya dini kuendelea kuweka mkazo mkubwa kufundisha masomo ya dini katika shule za msingi na sekondari ili kujenga kizazi chenye hofu ya mungu na hatimaye kuwa na jamii yenye uadilifu isiyojihusisha na matendo maovu.


Padre Maswenya alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili juu ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo ya kikatili katika baadhi ya mikoa hapa nchini.


Alisema kuwa somo la dini mashuleni lilikuwepo tangu zamani lakini bado hakuna mkazo wa kutosha kwa wahusika wanaopangiwa ,hivyo ni wakati sasa kwa viongozi wa dini kujikita kwa nguvu zote ili kulea kizazi hiki ambacho kwa sasa kinakabiliwa na changamoto kubwa ya utandawazi.



No comments