Ads

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA MAELEZO MABADILIKO YA TOZO




Na. Wellu Mtaki, Dodoma

Jeshi la zimamoto na uokoaji limesema kuwa      kuanzia mwezi julai ,2022 Kumekuwa na mabadiliko ya tozo na ukaguzi wa usalama dhidi ya majanga ya moto katika majengo na maeneo mbalimbali  pamoja na ukusangaji wa tozo.

Ameyasema hayo kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma.

"Tozo hizo zinakusanywa KWa mujibu wa sheria no 14 ya mwaka 2007 " The Fire and Rescue Force Act" ikisomwa pamoja na kanuni ya ukaguzi na vyeti ya mwaka 2008 pamoja na mabadiliko ya mwaka 2022" amesema Nzalayaimisi

Pia jeshi lina jukumu la kumfuata mteja na kumuomba kufanya ukaguzi kwenye jengo , eneo, au chombo cha usafiri Ili kuleta tija na kiliwezesha jeshi kutekeleza majukumu yake.

Aidha kanuni ya ukaguzi na vyeti immeelekeza kuwa ni wajibu wa mteja  au Mmiliki wa jengo , eneo, au chombo cha usafiri ambaye hajafanyiwa ukaguzi afike ofisin za jeshi la zimamoto na uokoaji kuomba kukaguliwa, hii ni KWa mujibu wa kanuni isemayo

" Any person Who is an Owner Or Operator of Premises, Vehicle Vessel or any other conveyance facility which has not been inspected and issued with fire safety certificate by fire authority shall apply in writing to the fire Authority for conduct of inspection in his premises,vehicle, vessels or any other conveyance facility.."


Pia jeshi la zimamoto linawajulisha imma mabadiliko ya gharama za tozo katika maeneo mengi mfano maduka, viwanda, makazi, ofisi, shule, nyumba za kuishi, usomaji wa ramani pamoja na grarama za usajili wa makampuni yanayojishughulisha na utoaji wa huruma za kuuza vifaa.


Nzalayaimisi amesema zipo tozo ambazo zimefutwa mfano Transformer , mashamba ya kahawa, mkonge pamoja na chai, 


Pia amewahimiza wamiliki wa majengo , eneo pamoja na vyombo vya usafiri kufatilia taarifa Ili kupata elimu , sheria na nyaraka zingine kupitia mitandao ya kijamii ( instagram @tanzimamoto, Twitter @tanzimamoto, Facebook @jeshi la zimamoto na Uokoaji ) na kuwasiliana kupitia namna zilizoainishwa KWa changamoto zote kuhudi mabadiliko hayo. 


Pia Nzalayaimisi amewakumbusha wanainchi kushiriki zoezi la sensa itakayofanyika tarehe 23 Agosti, 2022. 

"Sensa ni muhimu KWa maendeleo ya taifa katika jeshi la zimamoto na uokoaji itasaidia katika upandaji wa vitendea kazi pamoja na upandaji wa rasilimali watu katika vituo vya kazi.

No comments