Ads

WAZIRI BASHE ATEUWA KAMATI YA MKONGE.

 

NA: FARIDA SAID, MOROGORO.

Waziri wa kilimo Mhe. Hussen Bashe amemteuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bwana. Adam Malima kuwa mwenyekiti wa kamati ya zao la mkonge akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Martine Shigela lengo likuwa ni kufufua kwa kasi kilimo cha zao hilo kwenye mikoa inayofaa kulima mkonge ikiwemo Morogoro na Tanga.

Akizungumza mjini Morogoro Waziri Bashe alisema kamati hiyo imepewa kazi kubwa ya kufanya upembuzi yakinifu na kutoa majibu kwa serikali ni maeneo gani yanafaa kwaajili ya uzarishaji wa zao la mkonge pamoja na kutoa hamasa kwa wakulima wadogo.

Bashe alisema serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha zao la mkonge linapata thamani ambapo imetenga fedha ajili ya ujenzi wa maabara ya utafiti wa mbegu za mkonge katika kituo cha utafiti cha TARI MLINGANO kilichopo mkoani Tanga.

Aidha alisema wizara ya kilimo imeenza kufanya mazungumzo na ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira kuangalia namna ya kutunga kanuni itakayozuia mazao yote ya kilimo kushonwa na nyuzi za plastiki badala yake zitumike nyuzi za mkonge.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Morogoro bwana Martine Shigela alisema mkoa huo umejipanga katika kuzarisha mkonge kwani wameshaanza kuwatambua wakulima wadogo wa zao hilo pamoja na kuwapatia mbuge bora. 
   
Pamoja na kuwatambua wakulima wadogo Shigela alisema kama mkoa utafanya uhamasishaji kwa wakulima wengine ambao bado hawajaanza kulima zao hilo kwa kuwagawia mashamba ambayo yamefutwa umiliki wake na kurudishwa kwa wananchi na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ili wakulima hao waweze kulima zao la mkonge.

“Tunaenda kupima mashamba na kuwagawia wakulima wetu wote tena tunawapa bure na tutawapa maelekezo walime zao la mkonge ili tuweze kuwa na uhakika wa uzarishaji wetu.” Alisema Shigela.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaim Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya mkonge Tanzania Bwana Saddy Kambona alisema kuundwa kwa kamati hiyo ndogo kutaleta tija kubwa kwenye uzarishaji wa zao la mkonge kwani wakulima wadogo wanamchango mkubwa kwenye uzarishaji wa zao hilo.

Alisema moja ya mikakati ya bodi ya mkonge ni kutoa hamasa kwa wakulima wadogo waweze kulima zao hilo pamoja na matumizi sahihi ya teknolojia kwenye kilimo cha mkonge.

Uzarishaji na usambaji wa mbeguza mkonge kwa wakulima kwani serikali imeshatoa fedha kwaajili ya zoezi hilo lengo likuwa ni kuwafikia wakulima wadogo wengi zaidi kwenye mikoa ambayo inafaa kwajili ya kilimo cha mkonge. 

Aidha amewaomba wadau na wafanyabiashara kuchangamkia fursa iliypo kwenye zao la mkonge kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo vya kuchakata na kuliongezea thamani zao hilo kwani kwa sasa linatengeneza bidhaa nyingi sana.

Alisema wanatumia mbinu mbalimbali katika kuhakikisha wanafikia malengo ya uzarishaji ya tani laki moja na elfu ishirini ifikapo mwaka 2025.

No comments