WADAU WAPIGWA MSASA KUHUSU BIASHARA YA FOREX
Forex no biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ambao imeonekana kuwa na mzunguko mkubwa zaidi kuliko biashara yoyote duniani kwani inazungusha zaidi ya dolla za kimarekani trilioni 5 kwa siku.
Kwa kutambua hilo kampuni
ya udalali wa biashara ya forex,(Vault Market Tanzania)ambayo hutengenezwa
platform kwa wanaotaka kufanya(wanaofanya) biashara hiyo imemleta hapa nchini
mfanyabiashara maarufu na mwenye mafanikio kupitia biashara hiyo Joash Naidoo
kwa lengo la kutoa elimu juu ya biashara ya forex.
Amesema kampuni ya Vault
Markets yenye makao yake makuu nchini Afrika ya kusini tayari imefungua matawi
katika miji mbalimbali mikubwa katika nchi nchi tofauti barani Africa ikiwemo
Namibian na sasa jijini Dar es salaam nchin Tanzania na wana mpango wa kuenea
majiji yote hapa nchini.
Aidha amesema kuwa semina
hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na amewataka watanzania kujiridhisha na
biashara ya forex kwani ni moja ya biashara zenye mafanikio makubwa endapo
wataitumia kampuni ya Vault Market kama brockers wa 'forex trade'.
Post a Comment