Ads

BAYPORT ILIVYOJIPANGA KUWASAIDIA WATUMISHI WA UMMA.

 


Mdau wa Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Haji Manara (wa pili kutoka kulia) akisaini mkataba wa makubaliano ya kuwa Balozi wa Taasisi ya  Fedha ya Bayport Financial Services kupitia mradi wa kuwakopesha watumishi wa umma, (wa kwanza kutoka kushoto) Afisa Mkuu wa Uendeshaji Taasisi ya Fedha Bayport Bw. Nderingo Materu. 

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Watumishi wa umma nchini wametakiwa kuchangamkia fursa katika Taasisi ya Bayport Financial Services ambayo imezamilia kuwasaidia kwa kuwakopesha kiasi ya fedha kwa muda mfupi ndani ya saa 24 kwa kutumia njia ya simu ya mkononi.

Akizungumza leo tarehe 27/7/2022 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Balozi wa Taasisi ya Bayport Financial Services Bw. Haji Manara, amesema kuwa taasisi ya fedha ya Bayport inatoa mkopo kwa mashariti nafuu kwa ajili ya kuwasaidia watumishi wa umma kujikwamua kiuchumi.

Bw. Manara amesema kuwa Bayport ni taasisi ya kifedha ambayo imefata utaratibu na miongozo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa watumishi wa umma ili waweze kufikia malengo tarajiwa katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.  

“Mishahara yetu bado inatusaidia sana, lakini bado tunaitaji msaada kutoka Bayport na zamani ili upate mkopo utaratibu ulikuwa mrefu, lakini leo unatumia simu na ndani ya muda mfupi unapata mkopo wako” amesema Bw. Manara.

Ametoa wito kwa wachezaji wa mpira wa miguu nchini kutumia fursa ya mitandao ya kijamii vizuri kwa kujiingia kipato ili waweze kupunguza ukali wa maisha.

Afisa Mkuu wa Uendeshaji Taasisi ya Fedha Bayport Bw. Nderingo Materu, amesema kuwa wameamua kutoa mikopo kwa njia ya mtandao wa simu (digital) ili waweze kuokoa muda na kufikisha huduma kwa haraka kwa watanzania.

Bw. Materu amesema kuwa mtumishi wa umma anaweza kutumia simu ya aina yoyote kwa ajili ya kuomba mkopo kwa muda wa saa 24, ambapo ni utaratibu huo ni rafiki kwa kila mtu.

“Yapo maswali ambayo mtu anaweza kujiuliza, kweli naweza kupata mkopo bila kujaza popote? Jibu ni Ndio, kweli napiga simu tu Napata mkopo ?  Jibu ni ndio, fedha kweli nitapata?  jibu ni ndio, wewe tupigie simu kutupe ndiooo! zako” amesema Bw. Materu.

Mkuu wa Mauzo Taasisi ya Fedha Bayport Bw. Lugano Kasambala, amesema kuwa huduma ya mikopo kwa njia ya simu kwa sasa wanaitoa kwa watumishi wa umma, lakini baadaye wanafikilia kuanza kutoa huduma kwa watumishi wote.

“Tunaweza kutoa huduma ya mkopo ambaye sio mtumishi wa umma kwa kutegemeana na huyo mtumishi kwa mkataba ambayo tutaingia naye” amesema  Bw. Kasambala  

Kauli mbinu ya kufanikisha utoaji wa mkopo kwa njia ya simu kwa watumishi wa umma ‘Ndiooo!’ ambapo mtumishi wa umma anaweza kupiga namba *150*49# kupitia simu yake ya mkononi kwa ajili ya kupata mkopo, au anaweza kuongea na mtoa huduma wa Bayport kwa kupiga namba 0800782700 na kuzungumza naye.

No comments