Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine katika mji wa Mariupol wamesalimu amri.Kulingana na msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov, wanajeshi waliokamatwa ni 1,026 wa kikosi cha 36 cha Ukraine.
Konashenkov amesema miongoni mwa wanajeshi hao wanaowashikilia ni maafisa 162 na wanawake 47.
Konashenkov ameripoti pia mashambulizi mapya kutumia ndege na manuari za Urusi dhidi ya maghala mawili makubwa ya silaha nchini Ukraine.
Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Ukraine Oleksandr Motuzyanyk hata hivyo amesema hana taarifa yoyote kuhusu wanajeshi wa Ukraine kujisalimisha mjini Mariupol kama ilivyoripotiwa na Urusi.
Post a Comment