Urusi yaamuru uchunguzi wa mauaji ya raia Bucha
Mkuu wa upelelezi wa Urusi, Alexander Bastrykin ameamuru uchunguzi rasmi wa kile alichokiita uchokozi wa Ukraine, baada ya nchi hiyo kulishutumu jeshi la Urusi kuwaua raia kwenye mji wa Bucha.
Bastrykin ameamuru uchunguzi ufunguliwe kwa misingi kwamba Ukraine imeeneza habari za uongo makusudi kuhusu vikosi vya Urusi huko Bucha.
Urusi pia imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuandaa mkutano kwa kile ilichosema jaribio la Ukraine kuvuruga mazungumzo ya amani na kuzidisha ghasia kwa uchokozi wa Bucha.
Wakati huo huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuna dalili za wazi za uhalifu wa kivita katika mji wa Bucha uliyofanywa na vikosi vya Urusi.
Ujerumani imesema mataifa ya Magharibi yatakubaliana kuweka vikwazo vipya kwa Urusi katika siku zijazo.
Poland imetoa wito wa uchunguzi wa kimataifa kuhusu kile ilichokiita ''mauaji ya kimbari'' yaliyofanywa na majeshi ya Urusi.
DW
Post a Comment