Ads

Rais samia atoa ujumbe mzito kwa watumishi na viongozi





 Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan , amesema hali ya Utumishi wa Umma sio nzuri  na kwamba katika awamu ya tano baadhi ya Watumishi walisifiwa kwa heshima ambayo haikutoka moyoni bali ilitokana na uoga.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu,Chamwino Jijini Dodoma leo April 2-2022.

"Tunasifiwa kwamba adjustments tuliyoyafanya awamu ya tano imeleta heshima ndani ya utumishi wa umma, heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwasababu kulikuwa na Simba wa Yuda ambaye alikuwa ukigusa sharubu anakurarua lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja awe na itikadi moyoni kwake kwamba Mimi ni Mtumishi wa Serikali majukumu yangu ni haya, kila mmoja aheshimu laini ya mwenzie hicho tunakosa Serikalini"Amesema 

Aidha amewataka viongozi hao kufanye kazi kwa kufuata miongozo na sheria za nchi huku akisisitiza kuwa yeye sio Mtu wa kufokafoka bali atatumia kalamu kuwachukulia hatua wanaokosea.

"Msiende kuendekeza nafsi zenu, katika utendaji kazi 70% inachukua miongozo, dira na sheria za Nchi na 30% unasikiliza nafsi yako na nafasi yako ukiisikiliza ikupeleke kwenye malengo mazuri sio malengo mabaya wote lengo letu kukuza uchumi na ustawi wa Nchi yetu na kukuza jina la Tanzania, mkaheshimu viapo mlivyoapa"

"Huko nyuma nilisema sitofoka nitafanya kazi kwa kalamu, nitawakumbusha lakini sitofoka kwasababu hata ukinitazama sijaumbwa kufokafoka na Mimi ni Mama ni Mlezi nitajaribu kuwalea lakini ulezi utakaponishinda nitachukua hatua, niwaombe sana mkanisaidie sio mkaharibu mkanisaidie"


No comments