NDC ILIVYOJIPANGA KUTOKOMOEZA UGONJWA WA MALARIA
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani, Afisa Utawala na Rasirimali watu Mkuu wa Velentine Simkoko ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa NDC, amesema kwa sasa wanapitia njia mbali mbali ili kutokomeza mazalia ya mbu .
Velentine amesema wameweza kufanya maadhimisho hayo kwa kufika maeneo tofauti ikiwemo Mabibo, Jitegemee katika Mkoa wa Dar es Salaam na wameweza kunyunyizia dawa kuthibiti viluwiluwi kwenye maji yaliyotwama.
"Tumeweza kuadhimisha kwa kutumia viuadudu ambayo ni njia isiyo na madhara inayoangamiza vililuilui vya mbu wa aina zote, bila kuacha wala kusababisha madhara kwa viumbe hai wengine isipokuwa kiluwilui,"amesema Velentine.
Amesema NDC wanahakika taratibu za kutoa elimu itaendelea kuwafikia wananchi, hivyo kujivunia kutumia kiwanda cha kuzalisha viwadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu, Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) .
Amesema kuwa baadhi ya halmashauri nchini wamekuwa wakinunua na kutumia bajeti zao na wamekuwa wakiwasisitza halmashauri zingine kutumia viwadudu kuangamiza mazalia.
Afisa Masoko wa TBPL Magdalena Uisso, amesema kuwa wamefanikiwa kunyunyizia dawa Mabibo hasa katika maeneo yenye changamoto katika miundo mbinu mibovu ya barabara.
Mwenyekiti wa Mtaa huo Yusuph Abdullah, amesema kuwa amesifu juhudi hizo kwa kuwa zinaweza kuibua kutatua changamoto ya kutokomeza malaria
Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu, Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kilizinduliwa ramsi na Rais wa Awamu ya 4 Mh. Dkt. Jakaya M. Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, 2 Julai 2015 Kibaha.
Mjumbe wa Shina namba 10 Mabibo Oswin Carol Nungo, amesema kuwa wamefurahia kufikiwa katika maadhimisho ya malaria duniani ujio huo kwani eneo hilo, kihistoria lilikuwa mashamba baadaye wananchi wameweka miji, hivyo uhakika wa kuwepo mazalia ya mbu ni mkubwa.
Post a Comment