Ads

USIYO YAJUA KUHUSU VITA VYA UKRAIN NA URUS- ONEZA UELEWA HAPA

 



Vita ya Donbas (DONBAS WAR) maarufu kama RUSO-UKRANIAN WAR ni vita ambayo inaendelea kati ya Russia na Ukraine i.e vita hii inapiganwa katika ukanda wa Mashariki ya Ukraine katika miji miwili ya Donetsk na Luhansk (DONBAS REGION).


Tangu Russia waichukue rasmi Peninsula ya Crimea mwaka 2014 kutoka kwa Ukraine, Mgogoro mpya wa kutaka kujitawala kwa Miji miwili ya Donetsk na Luhansk ulianza rasmi. i.e Machafuko makubwa yalianza tangu Februari 2014.

Baada ya kuvutana kwa muda mrefu sana hatimae Russia na Ukraine wakakubaliana kukaa chini na kumaliza mgogoro huu, hapa walikuja na kitu kinaitwa MISK PROTOCOL mnamo mwaka 2014.

Mataifa ya Germany na France yalitumika kama wasuluhishi. Wahusika walikutana katika mji wa Minsk uliopo Belarus, mwishowe ilipofika tarehe 5 Septemba 2014 walisaini makubaliano ya kusitisha mapigano na utumiaji wa silaha za moto.

Makubaliano haya yalifeli kwani baada ya muda mchache mapigano yalianza kwa kasi sana, kikundi cha "Separatist Forces" kutoka Donetsk People's Republic (DPR) na Luhansk People's Republic (LPR) walianzisha mapigano mapya dhidi ya Majeshi ya Ukraine.

Mapigano ambayo yalivunja makubaliano ya awali ya "MISK I PROTOCOL". Hapa ndipo viongozi wakaitana tena na ilipofika Februari 2015 walikuja na makubaliano ya awamu ya pili ambayo yaliitwa "MISK II AGREEMENT".

Waliongeza makubaliano mapya huku wakikubalina kusitisha mapigano kwa kuondoa silaha za kivita, Ukraine alikubali kufanya mabadiliko ya katiba yao kwa kuiruhusu miji ya Donetsk na Luhansk kuwa huru na mengine mengi.

Mambo hayakwenda sawa, kwani mapigano yaliendelea na mwishowe vikundi vya "Separatist Forces" na "Pro Russian Army" walifanikiwa kuchukua robo tatu ya eneo la DONBAS.

Ulipoanza Mwaka 2022, Tarehe 21 Februari Russia ikaitambua rasmi Miji hii miwili ya Donetsk na Luhansk kama nchi zinazojitegemea. i.e Putin akasema Makubaliano ya Misk hayapo tena na hivyo Miji hiyo si sehemu tena ya Ukraine.

Siku tatu baadae ndo vita hii inayoendelea ilianza rasmi na mpaka sasa tunaona hayo yote ambayo yanatokea, lakini nyuma ya pazia kuna mengi sana kati ya hawa ndugu wawili.

No comments