TBS KUKUTANA NA WADAU KUJADILIANA UANDAAJI WA VIWANGO.
..........
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepanga
kukutana na wadau ili kujadiliana ushiriki wao katika shughuli za uandaaji wa
Viwango ambapo itafanyika kwenye ofisi za TBS Kanda Mkoa wa Arusha tarehe 29
hadi 31 Machi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es Salaam Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Massawe, amesema wameandaa mkutano wa
wadau wa sekta ya Utalii kufanya majadiliano kuona mchango wa viwango ukitumika
vizuri katika kukuza sektarisch hio. Pia maeneo gani ambayo yanaonekana
yanauhitaji wa Viwango.
Amesema watawakutanisha pia wadau wa umeme na
kutoa elimu katika Viwango vya nyaya za Umeme hususani katika eneo la mabadiliko
ya rangi za nyaya za umeme.
Ameeleza
kuwa kumetokea mabadiliko katika viwango rangi za nyaya za umeme lakini
utekelezaji wake umekuwa na changamoto, hivyo ni fursa pekee kwa wadau wa Umeme
kushiriki na kujadiliana njia bora ya utekelezaji wa Viwango husika.
“Tutawakutanisha watueleze ni changamoto gani
ipo lakini maeneo gani kama TBS tunahitaji kufanya viwango tuwekeze huko”.
Amesema Bw.Massawe.
Aidha Bw.Massawe amesema tarehe 31, Machi 2022
ambapo maadhimisho hayo yatakuwa tamati kwa Tanzania, watakuwa na na
kutaoneshwa kwa vitendo moja ya utaratibu wa kuandaa Viwango kupitia kamati za
kitaalamu. Kamati ya kitaalamu itakuwa na Kikao na namna ya majadiliano ya
kuandaa Viwango vya kitaifa na wageni waalikwa watakuwa kama wafuatiliaji.
Ameeleza kuwa siku hiyo kutakuwa na tukio
maalumu la ugawaji zawadi kwa washindi wa shindano la uandishi wa Isha kwa
wanafunzi wa elimu ya Juu, shindano ambalo lilianza Rasmi Novemba 25 , 2021
ambapo isha 223 zilipokelewa.
“Tumesahihisha hizi Isha 223 tukapata isha bora 10 ambapo wameeleza vizuri mchango wa Viwango katika kutatua changamoto mbalimbali za magonjwa ya milipuko, insha zimeeleza vizuri, viwango ni nini, changamoto mbalimbali ambazo zililikumba bara la Afrika katika kuagiza vifaa tiba na madawa katika kupambana na UVIKO -19 “. amesema
Post a Comment