Ads

Meya wa Ukraine atekwa na Jeshi la Urusi

 


moshi

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema meya wa jiji la Melitopol, ametekwa nyara jana Ijumaa, na wanajeshi wa Urusi. Jiji hilo kwa sasa linatajwa kuwa katika udhibiti wa vikosi vya Urusi.Katika ukurasa wa Twitter bunge la Ukraine pia limeandika "Kundi la watu 10 lilimteka nyara meya wa Melitopol, Ivan Fedorov," kwa kusema alikataa kutoa ushirikiano kwa yule waliemtaja kuwa ni adui.Katika ujumbe wake wa jana Ijumaa, kwa njia ya video Rais Zelensky alithitibisha kutokea kwa kitendo hicho, na kumsifu Fedorov kuwa ni mtu shujaa ambae anaitetea Ukraine na jamii yake kwa ujasiri mkubwa.Kwa mujibu wa bunge la Ukraine, afisa mwingine mwandamizi, ambae ni naibu kiongozi wa baraza la mkoa wa Zaporizhzhia, eneo la umbali wa kilometa 120 kutoka Melitapol, alitekwa lakini aliachiwa huru siku chache zilizopita.

No comments