Mazungumzo kurejea wakati Urusi ikiukaribia mji wa Kyiv
Wanajeshi wa Urusi wameendeleza harakati zao za kijeshi kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv wakati pande zote zikitarajiwa kukutana leo katika mazungumzo ya ana kwa ana.
Siku moja baada ya kutanua vita Ukraine kwa shambulizi kwenye kituo cha kijeshi karibu na mpaka wa Poland, mapigano yameendelea viungani mwa Kyiv.
Maafisa wa Ukraine wamesema wanajeshi wa Urusi walifyatua makombora nje ya mji huo mkuu ambapo raia wawili wameuawa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameitaka Jumuiya ya Kujihami ya NATO kutangaza amri ya kutoruka ndege katika anga yake.
Mshauri wa Rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak amesema maafisa wa Ukraine na Urusi wanakutana tena leo kujadili miongoni mwa masuala mengine, upelekaji wa chakula, maji na dawa pamoja na bidhaa nyingine katika miji na vijiji vinavyokabiliwa na mashambulizi.
credit DW
Post a Comment