IMF YAONYA VIKWAZO VIKALI DHIDI YA RUSSIA
Vikwazo vya kifedha ambavyo havijawahi kushuhudiwa vilivyowekwa dhidi ya Urusi baada ya kuanzisha operesheni ya kijeshi nchini Ukraine vinatishia kupunguza ‘utawala wa dola ya Marekani’ na kusababisha kugawanyika zaidi kwa mfumo wa fedha wa kimataifa, afisa wa ngazi ya juu katika Shirika la Fedha Duniani IMF ameonya.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Gita Gopinath amesema katika mahojiano na Financial Times kuwa hatua kubwa zilizowekwa na nchi za magharibi kufuatia operesheni ya Urusi, ikiwa ni pamoja na vikwazo kwa benki yake kuu, zinaweza kuhimiza kuibuka kwa makundi madogo ya fedha kulingana na biashara kati ya makundi tofauti ya nchi.
“Dola inaweza salia kuwa sarafu kuu ya kimataifa hata katika mazingira hayo, lakini kugawanyika kwa kiwango kidogo kwa hakika kunawezekana," Gopinath alisema siku ya Jumatano.
Aliongeza kuwa baadhi ya nchi tayari zinajadiliana upya kuhusu sarafu ambayo watatumia kwa biashara. Urusi na India kwa sasa zinatayarisha utaratibu wa rupee-ruble ambayo itaziruhusu kufanya biashara kwa sarafu za kitaifa huku zikikwepa dola.
Urusi imekuwa imekua ikifanya jitihada kwa miaka kadhaa kupunguza utegemezi wake kwa dola, kampeni ambayo iliongezeka kwa kasi baada ya Marekani kuweka vikwazo kufuatia uamuzi wa Urusi kuchukua eneo la Crimea mwaka 2014.
Post a Comment