WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI KUONGEZA NGUVU MABORESHA UTENDAJII WA TAZARA.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
.......
Serikali kupitia Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi imesema itatatua changamoto mbalimbali zilizopo katika
Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuendelea kufanya kazi zake kwa
ufanisi.
Akizungumza leo jijini Dar
es salaam wakati alipofanya ziara Shirika la TAZARA Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete, amesema Wizara yake itaunda Bodi Maalumu
ambayo itakua inashughulikia changamoto za TAZARA.
Amesema kuwa serikali ya
Tanzania na Zambia zimeanza kufanya mchakato wa kubadilisha sheria ili kufanya
marekebisho, kwani sheria iliyopo kwa sasa inazuia kufanya uwekezaji wowote
upande wa Tanzania bila kukubaliana na serikali ya zambia.
“Tunashindwa hata kuendeleza upande wetu wa
serikali kwa sababu sheria iliyopo inazuia kuwekeza chochote katika reli hii
mpaka tukubaliane na wenzetu, hivyo tayari mchakato wa kubadilisha sheria hii
unaendelea tukikamilisha hata baadhi ya changamoto zitapungua ”amesema Naibu
Waziri Mhe. Mwakibete.
Naibu Waziri Mwakibete
amesema kuwa shirika hilo linakumbwa na changamoto malimbali ikiwemo uchakavu
wa miundombinu , madeni makubwa ya wafanyakazi hali ambayo inachangia shirika kushindwa
kujiendesha kwa ufanisi mkubwa.
Amesema kuwa kuwa baadhi
ya wafanyakazi wa TAZARA hawapewi mikataba ya kudumu ya ajira hali ambayo
inawafanya wakose morali ya kufanya kazi, huku akisema kuwa suala hilo
linafanyiwa kazi na serikali.
Meneja Mkuu wa TAZARA
Tanzania Fuad Abdallah, amesema kuwa TAZARA inakumbwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo uchakavu wa miundombinu, upungufu wa mabehewa na injini ,madeni ya
wafanyakazi, madeni ya mifuko ya kijamii pamoja na madeni ya wasanbazaji .
Post a Comment