WIZARA YA AFYA YAKABIDHI MASHINE ZA KUCHANGANYA CHUMVI NA MADINI JOTO KWA TAMISEMI
Akizungumza wakati wa
kukabidhi mashine hizo kwa katibu mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, katibu mkuu
wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema Utafiti uliofanyika nchini mwaka 2019
ulibaini Tanzania inazalisha chumvi Tani 330,712 kwa mwaka na kati ya Chumvi
hiyo Tani 141, 22 ambapo ni sawa na asilimia 43 haiwekwi madini joto hivyo ujio
wa mashine hizo utasaidia kuongeza uzalishaji wa chumvi yenye madini hayo.
Prof Makubi amesema
mashine hizo ambazo zimetengenezwa nchini na wataalamu kutoka VETA zimeweza
kugharimu kiasi cha shilingi milioni 55 huku gharama ya mashine moja ikigharamu
kiasi cha shilingi milioni 11 na kusaidia kuokoa milioni 14 kwa kila mashine
endapo zingeagizwa kutoka nje ya nchi.
“Mwaka 2018 shirika la
Nutrition International ilifadhili ununuzi wa mashine tatu zilizoagizwa kutoka
Afrika Kusini kwa jumla ya Shilingi milioni 75 ambapo mashine moja iligharimu
shilingi Milioni 25 na kusimikwa Halmashauri za Kilwa, Hanang na Meatu na
zinaendelea kufanya kazi na safari hii mashine hizo zimeweza kutengenezwa na
Watalaam wetu kutoka VETA kusaidia kuokoa shilingi milioni 14 kwa kila mashine”
alisema Prof Makubi.
Awali akitoa maelezo juu
ya programu ya kuzuia upungufu wa madini joto nchini Mkurugenzi mtendaji wa
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna amesema Madini joto ni
moja ya kirutubisho muhimu kwa ukuaji mzuri wa akili na mwili wa binadamu na
endapo mtu atakuwa na upungufu wa madini joto basi anaweza kupata madhara
mbalimbali ikiwa ni pamoja na udumavu wa akili na mwili.
Dkt. Germana amesema
katika kukabiliana tatizo la upungufu wa madini joto Taasisi ya Chakula na
Lishe inatekeleza programu ya kuzuia upungufu wa madini joto nchini kwa kutumia
mkakati endelevu wa kuongeza madini joto kwenye chumvi (Universal Salt
Iodation) kuanzia miaka ya tisini na mkakati huo unalenga kuhakikisha kuwa
angalau asilimia tisini (90%) ya kaya zote nchini zinatumia chumvi yenye madini
joto ya kutosha kama inavyopendekezwa na shirika la afya duniani (WHO).
“Serikali kwa kupitia
Taasisi ya Chakula na Lishe kwa kushirikiana na wadau wengine tumefanya
jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa elimu na mafunzo kwa wazalishaji chumvi
kuhusu uzalishaji bora na uchanganyaji wa chumvi na madini joto, kuhakikisha
upatikanaji wa madini joto, kutoa vifaa
vya kupimia uwepo wa madini joto kwenye chumvi (Test Kits) na vile vya
kuangalia kiwango cha madini joto yaliyomo kwenye chumvi (WYD mashines).”alisema
Dkt Germana
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Nutrition International Dkt. Daniel Nyagawa amesema katika
Mpango mkakati wake wa miaka 6 ulioanza mwaka 2018 hadi 2024 shirika hilo
limejielekeza kufanya kazi zake kwa karibu na Serikali na Taasisi zake ili kwa
pamoja kuweza kupambana na utapiamlo na
madhara yatokanayo na utapiamlo.
Dkt. Nyagawa amesema kwa
sasa wanafarijika kuona sasa Mashine hizi zitaweza kupatikana nchini tena chini
ya Taasisi ya Serikali hivyo zoezi la ugawaji wa mashine hizi utakuwa endelevu
wakati wowote zikihitajika na kuna
uwezekano Tanzania ikavuka asilimia 61 ya kaya zinazotumia chumvi yenye madini
joto toshelevu endapo zitatumika kikamilifu.
Akizungumza kwa niaba ya
Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Katibu Mkuu Prof. Riziki
Shemdoe ameipongeza VETA kwa kuanza kutengeza mashine hizo kwa gharama nafuu
tofauti na zingeagizwa toka nje ya nchi na amewaagiza makatibu tawala wa mikoa
itakayopewa mashine hizo kuhakikisha
wanazitumia ipasavyo na siyo kwenda na kuzifungia stoo.
Nae Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Caroly Nombo amesema kutengenezwa
kwa mashine hizo na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) imejidhihisha kuwa sasa
wahitimu na wanafunzi wa vyuo hivyo vilivyopo nchi nzima sasa wameanza kutatua changamoto zinazoikabili jamii na
wanaweza kutengeneza vitu amavyo vitapatikana kwa gharama nafuu na kuokoa
gharama za fedha za serikali endapo bidhaa hizo zitaagizwa nje ya nchi.
Tanzania ina zaidi ya
wazalisha wadogo wa Chumvi 7000 wanaotumia teknolojia duni za kuzalisha chumvi
na wametawanyika katika maeneo mbalimbali
ambayo hayafikiki kwa urahisi hivyo ujio wa mashine hizi utasaidia kwa
kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha nguvu kinachozalishwa nchini bila kuweka madini
chumvi ya kutosha.
Post a Comment