Kadinali wa Ujerumani ashauri mapadri wa Katoliki waruhusiwe kuoa
Kadinali mmoja wa Ujerumani ametoa rai kwa Kanisa Katoliki kuondoa kigezo cha useja kwa mapadri wa Kanisa hilo.
Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Sueddeutsche Zeitung, askofu mkuu Reinhard Marx amesema mapadri wa Katoliki wangeruhusiwa kuoa ikiwa wanapenda kufanya hivyo.
Pia alitaja kigezo cha useja kuwa hatari lakini alikataa kuhusisha na visa vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo vimetikisa Kanisa Katoliki kote ulimwenguni.
Marx amejulikana kwa juhudi zake za kusukuma mageuzi ndani ya Kanisa katoliki.
Dayosisi yake iliyoko kusini mwa Ujerumani ilimulikwa katika ripoti iliyochapishwa mwezi uliopita juu ya unyanyasaji wa miongo kadhaa uliofanywa na mapadri.
Ripoti hiyo ilimtuhumu Papa Benedict XVI na Marx mwenyewe kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa unyanyasaji.
Matamshi hayo yanatolewa kuelekea mkutano mpya unaolenga kulifanya Kanisa hilo liwe la kisasa ifikapo 2023.
Chanzo DW
Post a Comment