Imamu Mkuu Msikiti wa Tambaza ahitimisha dua ya Rais
Na Dunstan Mhilu, Dar es Salaam.
IMAMU Mkuu
wa Msikiti wa Tambaza na Shehe wa Kata ya Upanga Magharibi Athuman Mohamed amehitimisha
dua ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan iliyodumu kwa siku saba.
Dua hiyo ilianza siku Rais
alipotimiza miaka 62, kama siku ya kumbukizi yake ya kuzaliwa na hivyo
wanafunzi wa Madrasa ya Tambaza walimuomba Imamu huyo kufanya dua maalumu
yakumuombea Rais.
Ameongeza kuwa maombi na
dua dhidi ya viongozi ni endelevu kikubwa wanaomba utulivu na amani uliopo
nchini uendelee kwani Mungu humpendeza zaidi kutuona tukiwa na amani na furaha
tele lakini Rais pia hutekeleza majukumu yake kikamilifu kukiwepo na amani.
Akiendesha Ibada hiyo
iliyokuwa rasmi kwa wanafuzi wa madrasa kumtakia heri Rais Samia alisema ni
ombi na ombwe la wanafunzi wa Madrasa ya Msikiti wa Tambaza kuomba kumfanyia
dua Rais.
“Ndugu waandishi wa Habari
leo hii tunahitimisha dua maalumu
tunawashukuru kushiriki pamoja nasi katika dua maalumu ya kumuombea Rais wetu
ili Mwenyezi Mungu kupitia Mtume (SAW) ampe heri na Afya njema ili atimize
kusudi la kiimani kuongoza nchi na wananchi wake”alisema
Aidha Imamu huyo alisema
kutimiza miaka 62 si jambo dogo ni umri mkubwa hivyo kutokana na umuhimu wake
kwa Taifa lazima viongozi wa dini wamfanyie du ana kumuombea kila wakati ili
afanye kazi zake kwa uhuru na umakini zaidi.
“Dua hizi na maombezi
huondoa dhoruba na sisi viongozi wa dini tumepewa jukumu lakuombea
nchi,Viongozi wa juu akiwemo Rais wake,wasaidizi wake na wote wenye mamlaka
hivyo tunatimiza takwa la kiimani” alisema
Kwa upande wao Wanafunzi
wa Madrasa hiyo walipata nafasi yakuzungumza baada ya Dua hiyo walisema kuwa
wanawapenda viongozi wote wa nchi na huwaombea kila siku ispokuwa juzi ilikuwa
ni siku maalumu kwa Rais kwasababu ni siku muhimu ya Rais.
“Sisi wajukuu zake wa
Madrasa ya Tambaza tunampongeza Rais kwakutimiza siku yake yakuzaliwa japo
tumempongeza leo wenzetu mbalimbali walimpongeza siku yake yakuzaliwa na sisi
tunamfanyia dua leo tunaamini hatujachelewa baada ya kumuomba Imamu wetu Shehe
Athuman na kutukubalia basi tunamuombe Maisha marefu kwa Mola afanye kazi bila
wasiwasi tunamuombea”alisema mmoja alisema Samira Mwanga
Naye Najash Sillia
mwanafunzi wa Madrasa hiyo alisema wanaguswa na jinsi Rais anavyosimamia haki
za Watoto ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo weanafunzi wote wa
darasa la kwanza na kidato cha kwanza wameanza masomo bila shida.
“Rais amewasaidia wazazi
wetu kwakugharamia ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati
kwani kila mwaka Januari wazazi walikuwa wakichangishwa hela za madawati lakini
sasa ndugu zetu wote waliopaswa kuanza la kwanza na kidato cha kwanza wameanza
bila shida.
Post a Comment