BINGWA MTETEZI KOMBE LA MAPINDUZI ATOLEWA KWENYE MASHINDANO
Mwamba wa Habari
Mwamba wa Habari
Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kutinga hatua ya fainali KOMBE la Mapinduzi baada kumfunga bingwa mtetezi ambaye pia ni Bingwa wa Kihistoria nchini ,Young Africans kwa changamoto ya mikwaju ya penati 9-8 baada ya kumalizika dakika 90 bila kufungana.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ambapo timuzote zilitosha nguvu kwa kucheza mpira unaovutia huku Yanga ikimkosa kiungo wake wa kimataifa Khalid Aucho na kipa wake wa kimataifa Didie Djiara.
Mchezaji wa Yanga Yassin Mustafa ndiye aliyekosa penati ambayo alipiga ikaenda juu hivyo mchezaji wa Azam Fc Mudathiri Yahaya akaweza kumalizia mpira wa mwisho na kuwapeleka fainali.
Azam Fc watawasubiri kati ya Namungo fc ama Simba Sc katika Fainali kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
Itakumbukwa Yanga mwakajana walitwaa KOMBE la Mapinduzi kwa kuwafunga Watani wao Simba SC na kuibua shangwe kwa muda wa Mwaka mzima ambazo zimezimwa Leo.
Post a Comment