Ads

Rais Samia Akutana Na Mjumbe Maalum Wa Waziri Mkuu Wa Uingereza Boris Johnson

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Mhe Rais Samia ameshawasili Glasgow kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Wengine katika picha wa kwanza (Kushoto) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberatha Mulamula na wa kwanza (kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. PICHA NA IKULU.


Mwamba wa habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 31 Oktoba, 2021 amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania Lord  John Walney.

Bw. Walney amekutana na Mhe. Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.

Amesema kukutana kwake na Mhe. Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamuwezesha kuwashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya bishara na utalii nchini Tanzania 

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Bw. Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Mhe. Rais Samia amesema Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.

 

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

No comments