MKUU WA MKOA WA RUKWA ASISITIZA ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA MKOANI RUKWA
Mwamba wa Habari
Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliomtembelea ofisini kwake
kwa ajili ya kuanza kampeni y utoaji elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango
25 Oktoba, 2021 mkoani Rukwa.
ofisini kwake kwa lengo la kumpatia taarifa kuhusu kuanza kwa kampeni ya utoaji
wa elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango.
Mhe Mkirikiti amesema kwamba TRA itapokua inafanya kampeni yake ya
kuwatembelea wafanyabiashara katika maduka yao wahakikishe kwamba
wanawapa elimu walipakodi kuhusu umuhimu wa wao kulipa kodi na kusikiliza
changamoto zao mbalimbali za kibiashara.
“Mkienda kufanya tathmini kwa walipakodi hakikisheni mnawaelimisha
walipakodi kwanini anapaswa kuvuka kwasababu baadhi yao hawana elimu ya
kodi na wengi wao wanaficha taarifa kwasababu biashara wanazofanya mtu hajui
hata biashara yake, anajua tu biashara yake kwenye kodi na masuala mengine”,
alisema Mkirikiti.
Ameongeza kuwa, angependa kuona TRA inakusanya kodi kutoka vyanzo
mbalimbali na kutoka katika makundi mbalimbali ambapo amefafanua kua katika
mkoa wake, kuna vyanzo mbalimbali vya kodi na pia ni mkoa wa pili katika mikoa
ya Nyanda za Juu Kusini kwa pato la Taifa ukiongozwa na mkoa Mbeya.
“Mkoa hauwezi kua na pato kubwa la Taifa wakati walipakodi wake ni wachache,
hivyo kuna mahusiano makubwa katika kazi mnazofanya TRA na hali halisi ya
mchango wa mkoa katika pato la Taifa”, alisema Mkirikiti.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA mkoani Rukwa, Bw. Fredrick Kanyilili ameeleza
kuwa, kampeni hiyo inalenga kuwatembelea walipakodi katika maduka yao ili
kuwatambua walipakodi ambao tayari wameshasajiliwa na kuwaelimisha kuhusu
masuala mbalimbali yanayohusu kodi ili walipe kodi zao kwa hiari.
Aidha, Mkuu wa msafara kutoka TRA Makao Makuu, Bw. Mackdonald
Mwakasendile amefafanua kuwa, ziara hiyo inalenga la kutoa elimu tu na sio
kwenda kuwakagua ama kuwatoza kodi wafanyabiashara wa mkoa wa Rukwa.
Kwa upande wao walipakodi mkoani hapo wameifurahia elimu ya kodi mlango
kwa mlango kwani wengi wao walikua hawajui masuala mbalimbali ya kodi na
wameiomba TRA kuwa na utaratibu wa kuwatembelea katika maeneo ya biashara
mara kwa mara kwasababu itawarahisishia wao kupata elimu hiyo kwa wakati
badala ya kufunga safari kwenda ofisi za TRA
Kampeni ya elimu kwa mlipakodi ni zoezi endelevu ambalo TRA inaendesha katika
mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa sasa zoezi hilo lipo katika mikoa ya Rukwa,
Ruvuma na Njombe na lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba elimu ya kodi
inawafikia walipakodi wote katika maeneo yao ili kodi stahiki iweze kukusanywa
ikiwemo kuwafanya walipakodi waweze kulipa kodi zao kwa hiari.
Post a Comment