MAPYA SHINDANO LA KUMTAFUTA MR. TANZANIA 2021.
Shindano la kumtafuta Mr.Tanzania limeendelea kupamba moto baaada ya waandaji kueleza kuwa maandalizi yote yamekamilika, huku wadau mbalimbali wakitakiwa kushiriki katika shindano hilo linalotarajia kufanyika siku ya Ijumaa October 22 mwaka huu katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi ya
Shindano hilo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF),
Bw. Francis Mapugilo, amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Bw. Mapugilo amesema kuwa
washiriki wote wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza saa 7:00 asubuhi
kwa ajili ya shindano la kumtafuta Mr.Tanzania 2021.
Amefafanua kuwa washiriki
wote wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 65 na wale watakaoshindwa
kufuata sheria za shindano hilo wataondolewa na kuzuiliwa kwa kuonekana kwenye
mashindano ya sasa na yale yajayo.
Katika shindano hilo mshindi
wa kwanza atachaguliwa kutokana na aina tatu zote za uzani Tsh.5m, mshindi wa
pili atachaguliwa kutokana na aina tatu zote za uzani Tsh.3m, huku mshindi wa
tat atachaguliwa kutokana na aina zote tatu za uzani wa Tsh.1m.
Utaratibu wa migandisho
hautakuwa zaidi ya sekunde 60 kwenye onesho la fainali, hivyo ni moja ya vitu
vya muhimu ambayo washiriki wanatakiwa kuvifaamu.
“Washiriki wanatakiwa kuzingatia na kuzielewa kanuni za mchezo huo ili
waweze kuchaguliwa kwani miongoni mwa vigezo vitakavyotumika ni kujua taratibu
na kanuni za mchezo huu” amesema Bw. Mapugilo.
Mchezo wa kutunisha misuli ni kama michezo mingine ambayo inaongeza
ajira kwa vijana, hivyo vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kushiriki.
Post a Comment