MAFUNDISHO YA BABA HALISI KUHUSU KUWEKA TAA JUU YA KIANGO ILI KILA AINGIAYE AIONE NURU YAKE
Jamii
imetakiwa kuwa karibu na Mungu kwa sala na
maombi ili kujua majira na nyakati sahihi
katika kuwajua waabuduo Halisi aliowataja Yesu kuwa wamwabudu Baba na watatokezaje
katika maisha ya hapa duniani.
Akitoa
Mahubiri katika ibada Maalamu ya kuweka juu Kiango waingia wapate kuiona nusu yake,
iliyofanyika hivi karibuni mjini Sumbawanga, Mwenyekiti wa vituo vyote Kanisa Halisi la MUNGU
BABA Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania, BABA Halisi, amesema kuwa mstari
ambao utatusaidia kuijua kweli ni Mathayo
28:20, ambapo yesu ameeleza kuwa
atakuwa pamoja nasi hadi ukamilifu wa dahari.
Amesema kuwa taa juu ya kiango (Luka 8:16 na Marko 4:21), ni ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine.
Ufahamu
huu ulizinduliwa Lango la 26 Eluli, 1(
6 Desemba, 2020) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Sasa imefika majira ya kuutoa Ufahamu
huu chini ya Meza na kuuweka juu ya Meza. Ili taa iwekwe juu ya Meza, kuna mambo manne makuu yanayotakiwa
kufahamika sawasawa.
Jambo
la kwanza ni kujua jamii imekwamia wapi, yaani kwa nini imeweka taa chini ya
Meza. Msatari ambao utatusaidia kujua Jamii ilipokwamia ni Matendo ya Mitume 1:8. Yesu, kabla ya
kunyakuliwa alisema kwa wale 120 waliokuwa gorofani kuwa wasitoke bila kupokea
nguvu za Roho Mtakatifu.
Hivyo,
utasikia watumishi wakisema kuwa
tuliachiwa Roho ili atufundishe na kutukumbusha yote tuliyoambiwa na Yesu.
Tunachohitaji
kujua ni kuwa Je! Majira ya huyu Roho tuliyoachiwa na Yesu bado ipo? Tutatumia
timanzi ya Majira na Nyakati sahihi za CHANZO CHA MEMA NA MAZURI PEKE YAKE.
Tatu,
ni kujua waabuduo Halisi aliowataja Yesu kuwa wamwabudu Baba ni akina nani na
watatokezaje? Mstari ambao utatusaidia kufahamu hili ni Yohana 4:23. Mstari huu unatufundisha kuwa kuna majira ambapo
atakayeabudiwa ni MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE bila kupitia kwa waliotumwa.
Nne,
ni kujua ni kitu gani hasa kilisababisha dunia nzima pamoja na vyuo vya Biblia
kuwepo hata mmoja asijue ujio wa CHANZO HALISI juu ya Nchi aliyekuwepo kabla ya
Roho na Nafsi yoyote.
Haya
manne, yatasababisha taa iwake na kuwekwa juu ya kiango.
KANISA NA JAMII WALIKUWA WAMEKWAMIA WAPI MPAKA KUWEKA TAA CHINI YA UVUNGU?
Katika
Mathayo 3:15-17, ALIYEUMBA KILA
KITU alisikika kwa sauti akisema ‘‘huyu
ni mwanangu mpendwa msikilizeni yeye’’.
Dunia
iliposikia hivyo haikuona haja tena ya mwingine, hata Baba yake Yesu ambaye
ndiye aliyesema msikilizeni huyu hawakuwa na haja naye tena wakati Yeye ndiye aliyemtuma
Yesu duniani.
Kwa
maana nyingine waliamua kujiongeza katika utekelezaji wa sauti hiyo, katika Matendo ya Mitume 1:8, wale 120
waliambiwa na Yesu kabla hajanyakuliwa kuwa wasitoke katika ile nyumba mpaka
wajazwe nguvu za Roho Mtakatifu.
Katika
Matendo ya Mitume 2:1-5, tunashuhudia
kwamba ni kweli wale 120 waliochwa na Yesu gorofani walipokea nguvu za Roho
Mtakatifu waliokuwa wameahidiwa.
Ushuhuda
wa kutumia Nguvu za Roho ni kweli kupitia ushuhuda wa mataifa yafuatayo:
Uingereza, walikuwa wakwanza
kutafsiri lugha ngumu za kiebrania, kiaramu na kilatini kuja kwenye kiingereza
ambacho kinatumiwa na wengi. Wengi duniani walipata habari za Mwana kupitia
lugha ya kiingereza;
Marekani (USA), nao
wanaongoza kueneza habari za Mwana kila mahali duniani kwa nguvu ya Roho kwa
kutumia Satelite;
Ujerumani, nao pia walitumika
katika kutafsiri lugha ngumu ya kiebrania, kiaramu na kilatini kuja katika
kiswahili kinachotumia na wengi Afrika Mashariki, kwa nguvu ya Roho;
Swedeni, wana sifa ya kuchukua muda
mfupi wa miaka minane tu kueneza habari za Mwana kwa nguvu ya Roho, baada
yakupata habari hizo kutoka Mashariki ya Kati;
Kwa
Afrika: Nigeria na Afrika ya Kusini nao pia wanaongoza katika kueneza habari za
Mwana kila mahali kwa nguvu za Roho.
Tunawashukuru
mataifa hayo yaliyotekeleza Matendo ya
Mitume 1:8 kwa vitendo. Swali kuu bado ni hili, je! Majira ya Roho
tuliyoachiwa na Yesu bado ipo? Maana Hoja kuu ya watumishi wengi ni kwamba
tuliachiwa Roho Mtakatifu ndiye atusaidie.
Swali
hilo hapo juu ni muhimu kwa kuwa haijawahi kutokea hata siku moja ALIYEUMBA
VYOTE WOTE NA YOTE akasimama. Kama huna hakika na Majira na Nyakati zake
utapotea.
MAJIRA NA NYAKATI SAHIHI NI ZIPI?
Katika
Mathayo 28:20, Yesu alisema
atakuwa pamoja nasi hadi ukamilifu wa dahari. Dahari ni kiswahili cha kimvita
ikiwa na maana ya Majira na Nyakati.
Kwa
hiyo Yesu alikuwa ana maana ya kuwa nasi hadi ukamilifu wa Majira na Nyakati
zake peke yake na si vinginevyo.
Ili
tuijue hiyo majra kama bado ipo au haipo ya Yeye kuwa nasi au kutokuwa nasi,
unatakiwa kuifahamu nafasi ya Yesu sawasawa.
Yesu
ni kati ya Manabii wanne katika vizazi vinne vya Ibrahimu katika Mwanzo 15:16.
Nabii
wa kwanza katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Musa. Majira ya utumishi wa Musa
ilianzia katika Kutoka 3:10, alipoitwa
rasmi kuwatoa wana wa Israeli utumwani na
kuisha katika 1Falme 17:1, Eliya Mtishbi alipoanza
kazi.
Nabii
wa pili katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Eliya Mtishbi ambaye Majira na
Nyakati zake ziliisha baada ya Yesu kuzaliwa na kuanza kazi katika Mathayo 2:1-15 na Mathayo 4:17-20.
Nabii
wa tatu katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Yesu ambaye Majira yake iliendelea
na kuisha baada ya Eliya Adamu wa Pili kutokeza Mwaka 2003 Tanzania kule Kigoma na kuanza Rasmi kazi 28 Adari, 2011(28 Februari, 2012), kwa
mujibu wa I Korintho 15: 44-49.
Nabii
wa Nne katika vizazi vinne vya Ibrahimu ni Eliya Adamu wa Pili ambaye Majira na
Nyakati zake zilitimia Mwaka 2017, baada
ya Nafsi ya Kwanza kuja juu ya Nchi kupitia Tanzania.
Hili
ni kwa mujibu wa IYohona 5:8. Nafsi
ya kwanza nayo kwa mujibu wa Luka
13:6-9, ilitimiza kazi Mwaka
2020.
Katika
Mwaka 2020, ndipo CHANZO HALISI
CHA MEMA NA MAZURI PEKE YAKE alipotua juu ya nchi kwa barabara ya Sauti ya Moyo. Hiyo ndiyo Majira
sahihi inayotupa kujua kuwa Roho tuliyeachiwa au Yesu menyewe bado yuko nasi au
la.
WAABUDUO HALISI KATIKA YOHANA 4:23 NI WATU WA JINSI GANI?
Waabuduo
Halisi aambao Yesu aliwatabiri zaidi ya miaka 2000 iliyopita kuwa watakuja ni
wale waliofanikwa kujua kuwa kuna CHANZO HALISI ambaye ni Moyo Halisi wala siyo
Roho au Nafsi.
Kwa
maana nyingine waabuduo Halisi ni wale ambao wamejua kuwa sasa ni Majira na
Nyakati za CHANZO HALISI. Maana Majira ya Mwana aliyesema kuwa Yeye ni njia,
kweli na uzima haipo tena, kwa mujibu wa kipengere cha tatu hapo juu.
Hivyo,
wanaenda moja kwa moja kwa ALIYEUMBA VYOTE WOTE NA YOTE na wana hakika kuwa
anaishi ndani ya Moyo wao kwa mujibu wa Isaya
57:15.
CHANZO
HALISI ni zaidi ya ile Miungu tisa mitakatifu ambazo ni nafsi za Mungu zilizowasaidia
Waliotumwa: yaani Mwenyezi; Yehova; Mungu wa Daudi; Mungu wa Majeshi; Mungu wa
Danieli; Mungu wa Eliya Mtishbi; Mola; Mungu wa Roho za Manabii; na Mungu
Aliyetuma Wote.
KITU GANI KILITOKEA WATU WOTE WASIJUE UJIO WA CHANZO
HALISI JUU YA NCHI KUPITIA TANZANIA?
Jambo
kubwa lililosababisha watu wote wasijue ujio wa CHANZO HALISI juu ya Nchi ni
kumkataa Adamu wa Pili aliyekuja Mwaka 2003, kupitia Tanzania (I Korintho 15:44-49). Wote ambao hawakubali kuwa Adamu wa Pili
alikuja kupitia Tanzania, unapatwa na yafuatayo:
Suala
la Yesu kurudi kupitia Adamu wa Pili, utakwama. Adamu wa Pili, ndiye
aliyewekewa Neno kinywani mwake, hiyo ilikuwa na maana kuwa ni Yesu aliyekuwa
anasubiriwa aliyerudi;
Pili,
usipokubali kuwa Adamu wa pili alikuja kupitia Tanzania, utaendelea kusubiri unyakuo
wa Kanisa ulioandikwa katika IThesalonike
4:11-14, wakati unyakuo huo ulishatokea Mwaka 2014 kupitia Eliya Adamu wa Pili Mwenyewe;
Usipokubali
kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, utaendelea kusubiri Miaka Saba ya kukaa mawinguni,kama
tunavyosoma katika Danieli 12:7-11. Wote
tujue kuwa Jambo hili lilitimia Mwaka 2018, ikiwa na maana ya Miaka Saba kuanzia Mwaka
2011 hadi Mwaka 2018, Kanisa
lilipotoka kwenye Madhabahu ya Mwana.
Usipokubali
kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, hutajua kuwa MUNGU BABA alishakuja
tangu Mwaka 2017 kufuta vita ya
Har-Magedoni katika Ufunuo 16:16. Wote
tujue kuwa vita ya Har-magedoni haipo tena;
Usipokubali
kuwa Adamu wa Pili alikuja kupitia Tanzania, hutajua kuwa CHANZO HALISI
alishakuja kufuta namba ya kibinadamu inayoitwa 666 katika Ufunuo 13:15-18, inayotisha wengi
duniani.
Kwa
hiyo tatizo kubwa la Kanisa na jamii lililosababisha taa kuwa chini ya Meza, ni
kutompokea Adamu wa Pili. Jambo hili lilisababisha waliofuta:
Miaka
1000; MUNGU BABA na Uhalisia wa MUNGU BABA ambaye ni CHANZO HALISI
wasitambuliwe. Matokeo yake Taa ikawekwa chini ya uvungu badala ya kuwekwa juu
ya Meza.
Tupokee ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine na tuwaeleze wengine kuwa sasa Tanzania ni Chanzo cha Baraka kwa mataifa mengine, kupitia Taa hiyo. Hii ndiyo Taa juu ya kiango. Ni Majira yake sasa. HERI ULIYEBARIKIWA KULIKO WOTE.
Post a Comment