DIT KWA KUSHIRIKIANA NA TDS YAWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WA SEKONDARI MKOANI MARA.
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa
kushirikiana na Tanzania Development Service (TDS) ya nchini
Marekani wametoa mafunzo ya kompyuta kwa wanafunzi 26 kutoka shule tatu za
Sekondari mkoani Mara.
Shule hizo ni pamoja na Sekondari ya Nyegina, Mugango
na Chief Wanzagi ambapo wanafunzi wameshiriki kwenye mafunzo hayo
yatakayotolewa kwa siku tano.
Mafunzo haya yanayoenda sambamba na ufungaji wa
kompyuta 30 yanatolewa na wataalamu pamoja na wanafunzi kutoka chuo Cha DIT.
Imeelezwa kuwa huo ni muendelezo katika kutekeleza
dhana ya mafunzo vitendo (Teaching Factory) inayotekelezwa na Chuo Cha DIT
ambapo wanafunzi wanapata mafunzo kwa vitendo zaidi ya yale ya darasani.
Matarajio ya DIT na TDS ni kuwa, baada ya mafunzo haya
wanafunzi wataweza kupeleka utaalamu huo kwa wengine ambao hawakupata fursa ya
kushiriki mafunzo haya.
Pamoja na kupata mafunzo wanafunzi, pia shule hizo wamepewa kompyuta 30 ambazo zimefadhiliwa na Taasisi ya TDS.
Post a Comment