Ads

DIT YATOA MAFUNZO YA KIHANDISI 'SOLIDWORKS' KUTENGENEZA MAUMBO HALISI 3D

 

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Prof. Preksedis Ndomba akizungumza na wanafunzi wa DIT kabla ya mafunzo hayo kuanza katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

.............

Wanafunzi 20 wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) leo wameanza mafunzo ya ya wiki tatu ya program za kihandisi (solidworks)  zinazotumika katika kutengeneza maumbo halisi (3D). Vilevile watajifunza jinsi ya kutumia machine zinazo tengeneza kifaa halisi (3D printers).

Mafunzo hayo yatakayoendeshwa DIT yamefadhiliwa na Shirika la Uratibu na Ushirikiano la Uturuki (TIKA)

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Prof. Preksedis Ndomba akizungumza kabla ya mafunzo hayo kuanza amesema kuwa,  lengo la mafunzo hayo ni  kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi na kuwataka watumie muda wao vizuri ili kuhakikisha wanapata ujuzi utakaowasaidia

"Mafunzo haya yanalenga kuwanoa zaidi kwenye masuala ya bunifu hivyo mjitahidi kufatilia kwa makini mwisho wa siku mtoke hapa mkiwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa vitendo zaidi na siyo kuhitimu tu chuo."amesema.

Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Viwanda, Dkt. John Msumba ameishukuru TIKA kwa kukubali kushirikiana na DIT kwa kutoa mafunzo hayo, amesema anaamini mafunzo hayo yatafungua fursa kwa vijana kuweza kujiajiri watakapohitimu.

Mbali na mafunzo hayo ya wiki tatu, TIKA itatoa pia vifaa ambavyo vitaendelea kutumika DIT kwa ajili ya kufundishia.

No comments