Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
.......................
Mratibu
wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo
Olengurumwa amesema kwa mujibu wa katiba na sheria za kimataifa mwenye jukumu
la kulinda haki za binadamu ni serikali pamoja na taasisi zake zikiwemo mahakama
pamoja na jeshi la polisi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tanzania
(THRDC) Bw. Onesmo Olengurumwa amesema kuwa ni vyema haki za binadamu
zikaendelea kuheshimiwa ili ziweze kusaidia kuitetea jamii katika changamoto
mbalimbali wanazokumbana nazo.
"Tunafahamu
kwamba ulinzi wa haki za binadamu mwenye jukumu la kwanza la kulinda haki hizo
kwa mujibu wa katiba na sheria za kimataifa ni serikali zetu na taasisi zake na
ndio maana tuna polisi,"amesema Olengurumwa .
Imeeleza
kuwa Taasisi za haki za Binadamu zikizingatia misingi ya kikatiba na kisheria
na haki za binadamu zitasaidia kulinda haki hizo na kuondoa changamoto kwa
jamii.
Amesema
ni vyema haki za binadamu zikaendelea kuheshimiwa ili ziweze kusaidia kuitetea
jamii katika changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Mohamed Hamis Hamad amesema ili kuzilinda
haki za binadamu ni vyema taasisi za kiserikali zikatumia nafasi zao katika
kuzisimamia taasisi.
"Ukizungumza
Haki za binadamu unazungumza kuishi katika mazingira mazuri, afya,kuishi, chakula
hivyo ukikivunja kimoja kinakuplekea katika mazingira mengine kwa hivyo kwa
misingi hiyo kuna haja ya kuimarisha juhudi za pamoja baina ya serikali na
wadau wote wa haki za binadamu,"amesema Mohamed
Mkutano
na mafunzo ya siku tatu inayohusisha Mtandao wa Taasisi za haki za Binadamu
Afrika wakijadili la Marakeshi ambalo limeweka utaratibu mzuri wa kulinda haki
za binadamu.
Post a Comment