Ads

OUT kilivyokusudia kutoa elimu bora kwa wahitimu wenye sifa kidato cha sita watakao kujiunga na masomo 2021/2022

Mkurugenzi wa Mahusiano Masoko wa chuo hicho Dkt. Mohamed Maguo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kinawakaribisha wahitimu wenye sifa wa kidato cha sita, Astashahada kujiunga na masomo ngazi ya shahada katika programu mbalimbali kwani chuo hicho kina mifumo thabiti ya usomaji na ufundishaji ikiwemo kwa njia ya mitandao.

Wanafunzi watakao jiunga na kozi mbalimbali katika Chuo cha OUT watapata faida ya kusoma na kujifunza kwa vitendo kwa kutumia miundo mbinu bora na rafiki kwa kila mwanafunzi .

Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mahusiano Masoko wa chuo hicho Dkt. Mohamed Maguo katika
maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwenye viwanja vya mnazi mmoja .

Dkt. Maguo amesema kuwa watakaojiunga na programu mbalimbali katika chuo hicho watapata faida ya kusoma kwa kujifunza kwa vitendo kwa kutumia miundo mbinu bora ikiwemo kupitia tehama.

"Kuna matawi ya OUT kwa kila mkoa ambapo mwanafunzi hana haja ya kuja makao makuu, anasoma na kujifunza mahali popote na tuna walimu waliobobea, mifumo bora ya ufundishaji hasa ya kwa nja ya mitandaoni ," amesema Dkt.Maguo.

Amesema kwa kutumia nyenzo hizo wahitimu watakuwa wenye sifa katika soko la ajira katika maeneo tafauti ndani nan je ya nchi.

Ameeleza kuwa OUT pia kinawakaribisha wanafunzi wa kidato cha sita na ngazi zingine waliopungukiwa sifa ya kujiunga na shahada ya kwanza kusoma kozi ambayo itamwezesha kuelendela na masomo yake ngazi ya juu.

Dkt. Maguo alisisitiza kwa wahitimu wa kidato cha nne wasio na sifa wanapewa nafasi kujiunga na OUT kwa kupitia kozi maalamu na watakapomaliza watakuwa na uwezo kusoma ngazi ya cheti katika chuo chochote.

Alifafanua kuwa mhitimu wa kidato cha sita aliyepata daraja la tatu la pointi 14 atalazimika kusoma kozi hiyo (Foundation Course) kwa mwaka mmoja ndipo wataendelea na masomo ya Shahada ya kwanza, huku wale waliomaliza Astashahada waliopata chini ufaulu wa G.P.A ya 3.0 watasoma kozi hiyo.

“Pia kozi hiyo ni pamoja na waliomaliza ngazi ya cheti NTA level 5
waliosoma miaka mitatu wataingizwa kwenye kozi, kwani chuo kilianzishwa mwaka 1992 kwa sheria No. 17 ya
Bunge inayokipa maelekezo ya kutoa elimu ya Juu kwa njia huria na masafa na kusisitiza bado kuna nafasi nyingi za kujiunga pasipo gharama yoyote ya maombi” amesema Dkt. Maguo.

Ameeleza kuwa wahitimu wa kidato cha sita,Astashahada, cheti
waliokosa sifa ya kujiunga shahada ya kwanza watalipia ada ya Sh 720,000 kwa kozi ya mwaka mmoja itakayomwezesha kujiunga shahada ya kwanza (Foundation Course), huku waliomaliza ngazi ya cheti  watalipa sh milioni 2.4.

Dkt.Maguo amesema kwa mwaka jana wa masomo 2020/21 waliweza kudahili wanafunzi 16,000 mpaka 20,000 na kwamba chuo hicho kina wanafunzi 60,000, huku wanaosoma ana kwa ana wahitimu ni 20,000 na 40,000 ni wale wanaoahirisha mwaka wa masomo.

Dkt. Maguo amesema  chuo cha OUT kina program zaidi ya 100 kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya Uzamivu pamoja na kozi takribani 1,000.

Amesema kuwa wanafunzi watakaosoma OUT watapata fursa ya kujisomea kupitia maktaba ya mtandao kwa ruhusa kuingia pale anapolipia ada na  ratiba ya mafuzo ya ana kwa ana kwa wanafunzi wenye vikwazo watakutana na walimu wao popote walipo.

Amesema kuwa wanafunzi wa chuo wameunda makundi ya mtandaoni ya majadiliano ya programu mbalimbali (Whatsapp discussion) ambapo kuna viongozi ndani yake hujadiliana masomo na pale panatokea changamoto huwasiliana na walimu wao.

Dkt. Maguo amesema makundi hayo yatawaunganisha wanafunzi wanaosoma OUT kujifunza mtandaoni na wamepewa jina la WhatsApp ni kimbweta kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Amesema wanafunzi wa utumiaji wa What's App kama Kimbwette cha kufanyia majadilianoya masomo yao ili kuwasaidia kuwaweka sawa.

No comments