MEYA KUMBIMOTO NA DIWANI SULTAN WAWEKEZA SEKTA ELIMU
Meya wa Halmashauri ya Jiii la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akitoka kukagua eneo la ujenzi wa shule ya Msingi Olimpio Leo Juni 21/2021 katika shule hiyo wamechanga Jumla ya shilingi mililioni 100,900,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya ghorofa 4(katikati)Diwani wa Upanga Mashariki Sultan Salim na Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji Saddy Kimji (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na HERI SHAABAN
MEYA wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto Diwani Sultan Salim , wawekeza katika sekta ya Elimu kwa kuanza na Dua Maalum kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Olimpio.
Dua Maalum ya ujenzi wa ghorofa NNE ya shule ya Msingi Olimpio iliongozwa Jana Juni 21/2021 na Shekhe wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu shuleni hapo.
Akisoma Dua hiyo shekhe wa Wilaya Adam Mwinyipingu aliomba kwa mwenyezi Mungu mafundi awafanyie wepesi ujenzi usimame kwa wakati ili watoto waweze kusoma .
Pia shekhe wa Wilaya aliomba kamati ya Shule na wasimamizi kusimamia ujenzi huo.
Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya jiji Omary Kumbilamoto aliipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri matokeo ya mwaka 2020 ya elimu ya msingi .
Meya Kumbilamoto alipongeza Kamati ya shule hiyo Diwani wa Upanga Mashariki Sultan Salim ,Mkurugenzi wa Jiji ,Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Katibu Tawala kwa kuwasimamia Wazazi wa Shule hiyo vizuri na kufanikisha kujenga ghorofa NNE katika shule hiyo
Meya Kumbilamoto alisema wanaunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu kuakikisha watoto wote wanapata elimu.
Alisema Taifa lolote ili liweze kuendelea na kupata maendeleo lazima wananchi wake wasome.
Alisema halmashauri hiyo inatekeleza agizo la Serikali mpango wa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.
Diwani wa Upanga Mashariki Sultan Salim alisema anasimamia katika sekta ya elimu kuakikisha ndani ya Kata hiyo elimu inakuwa na watoto wote wanasoma.
Pia Diwani Sultan Salim alisema vipaumbele vyake vingine katika kata hiyo kuisaidia Serikali katika suala zima la ukusanyaji mapato ili Serikali ifikie malengo yake kuendeleza miradi ya maendeleo.
Post a Comment