Ads

YAPO MALALAMIKO YA WALIMU WANAOJITOLEA KUWA NA BARUA FEKI ,WAZIRI UMMY:




Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema yapo malalamiko kuwa baadhi ya Walimu wanaojitolea wanawasilisha barua feki zinazosema wanafanya hivyo wakati hawajitolei

Ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2021 Bungeni Dodoma wakati akimjibu Mbunge wa Longido aliyehoji ni kwanini Seikali isiajiri Walimu ambao wanajitolea

Amesema hata Wanaojitolea watafanyiwa uchambuzi ili kuona kama ni kweli wanafanya hivyo akiongeza, kigezo kikubwa kitakachotumika katika utoaji wa Ajira ni hicho

Ameeleza, suala hilo ni tete ambapo nafasi ni 6,949 ilihali mpaka Mei 23, 2021 walioomba ni 89,958. Ameomba Serikali iaminiwe akisisitiza Haki itatendeka


No comments