Ads

WAZIRI JAFO ATOA MUDA UONGOZI WA KIWANDA CHA QUAIM STEEL MILLS KUDHIBITI MOSHI UNAOTOKA KWENYE KIWANDA HICHO.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa kiwanda cha Quaim Steel Mills limited mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akisikiliza maelekezo kutoka kwa baadhi  ya viongozi wa kiwanda cha Kamel Steel Industry kinachozalisha nondo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amekiagiza kiwanda cha Quaim Steel Mills limited kuhakikisha kufikia miezi  miwili kiwe kimejitengenezea mkakati wa kuhakikisha moshi wa kiwanda hicho hautoki na kusambaa kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Ameyasema hayo leo Mhe.Jafo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika viwanda vinavyozalisha nondo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Jafo  amewaagiza wenye kiwanda hicho kuhakikisha wanakifanyia marekebisho kiwanda hicho kwaajili ya kulinda afya za wananchi hususani ajenda ya utiririshaji wa moshi hivyo amewataka NEMC baada ya miezi miwili kufika katika kiwanda hicho na kukagua kama kimeshafanyiwa marekebisho.

“Kiwanda cha Quaim Steel Mills limited nimewapa miezi miwili waweze kufanya marekebisho makubwa katika kiwanda chao kwa lengo la kukidhi  sheria ya mazingira no.20ya mwaka 2004”. Amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo mewataka wenye viwanda nchini kuhakikisha wanazingatia afya za wananchi kwa kuhakikisha viwanda hivyo  havitirirshi moshi ama maji taka ambayo yataenda kuathiri watanzania.

Hata hivyo Waziri Jafo amesema atakaa na kuzungumza na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha wanavisaidia viwanda vya ndani viweze kufanya kazi vizuri na kuhakikisha mazingira yanatunzwa na vijana wa kiktanzania kupata ajira kupitia viwanda hivyo.

No comments