CCM Yalaani alichokifanya Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimelaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya
viongozi wa UWT mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum
Catherine Magige, baada ya kwenda kuvunja geti na kuingia kwenye
makaburi ya familia mahali ambapo amezikwa Kuzula Madoda anayedaiwa kuwa
mchumba wake.
Taarifa ya kulaani kitendo hicho imetolewa leo Mei
28, 2021, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Shaka
Hamdu Shaka, na kusema kuwa CCM inaamini katika kujenga uimara wa
familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia
halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.
"Chama
kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya
CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote
watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa Katiba,
kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya
CCM," imeeleza taarifa hiyo.
Haya yote yanajiri baada ya video
kusambaa mitandaoni zikimuonesha Mbunge huyo pamoja na watu wengine
wakitumia nguvu kushiriki katika mazishi ya mfanyabishara huyo mkoani
Arusha
Post a Comment