Wadau wa EAC wakutana kujadili mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wadau mbalimbali wanaojihusisha na maswala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki wamekutana kujadili namna ya kukamilisha uandaaji wa mikakati ya nchi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ,na kuwashirikisha wadau kutoka nchi za jumuiya hiyo , Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi nchini Tanzania(CAN-Tanzania)Dokta Sixbert Mwanga alisema kuwa,lengo la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau hao ili kuangalia hatua zilizofikiwa na kubalidishana uzoefu katika mchakato wa kuandaa kimkakati hiyo ambayo inatakiwa kukamilishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Dokta Mwanga alisema kuwa,katika mkutano wa maswala ya mabadiliko ya tabia ya nchi uliofanyika nchini Paris mwaka 2015 ulielekeza kila nchi kuhakikisha inakuja na mkakati yanayolenga kupunguza hewa ukaa na kuongeza ustahimili katika swala zima la mabadiliko ya tabia ya nchi kufikia mwaka 2020.
"Kutokana na changamoto ya Covid nchi nyingi zimeshindwa kutimiza lengo hilo kutokana na vile vizuizi vya mikusanyiko na kusababisha fedha nyingi kuelekezwa kwenye janga hilo ,hivyo mkutano huo umewaleta pamoja katika kuangalia hatua zilizofikiwa , changamoto ,pamoja na kubaini namna ya kushirikiana katika kutatua changamoto zilizopo ili kufanikisha ukamilishaji wa mikakati hiyo kabla ya mkutano mkuu wa kimataifa uliopangwa kufanyiwa mwaka huu nchini Uingereza.
Aidha mkutano huo ambao umefadhaliwa na serikali ya Ujerumani (BMZ) kupitia shirika la CARE Ujerumani pamoja na CAN -Tanzania pamoja na wadau wengine wakiwemo jumuiya ya Afrika mashariki na UNDP .
Naye Mkuu wa mazingira na maliasili jumuiya ya Afrika mashariki,Mhandisi Ladislaus Kyaruzi alisema kuwa,wanataka kuhakikisha kuwa nchi zote za jumuiya ya Afrika wanashirikiana kwa pamoja katika swala zima la utunzaji wa mazingira katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kyaruzi alisema kuwa,kupitia mkutano huo wadau kutoka nchi za jumuiya wataweza kuzungumza hatua walizofikia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuweza kupata uzoefu namna walivyofanya katika kukabiliana na mabadiliko hayo pamoja na kuwepo kwa changamoto ya COVID.
Kwa upande wake ,Mtaalamu wa miradi kutoka UNDP,Abbas Kitogo alisema kuwa,nchi ya Tanzania imeathirika Sana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,hivyo wadau hao wamekutana katika kujenga uwezo na uelewa namna ya kuweza kukabiliana na mabadiliko hayo na kuweza kujifunza kupitia kwa nchi wanachama wa jumuiya .
Kitogo alisema kuwa,UNDP ni kiongozi katika maswala ya mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo wanasaidia pia katika mkakati na kutekeleza malengo ya Taifa ya kushiriki katika kupunguza hewa ukaa duniani.
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Maliasili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,Mhandisi Ladslaus Kiyaruzi akizungumza na wadau wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi Jijini Arusha (Picha na Jane Edward Michuzi TV, Arusha)
Post a Comment