UFAFANUZI KUHUSU KUONDOA VIBANDA VYA WAFANYABIASHARA (WAMACHINGA) WALIOPO KANDOKANDO YA BARABARA
Dar es Salaam,
Kufatia tangazo lililotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 07/05/2021 kuhusu kuondoa vibanda vya wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) waliopo kandokando ya barabara,
Ufafanuzi wa tangazo hilo lililotangazwa kwa njia ya gari ni kama ifuatavyo kwamba vibanda vinavyotakiwa kuondoshwa ni vile vilivyojengwa kwenye barabara za watembea kwa miguu na juu ya mifereji ya maji ya mvua katika eneo la katikati ya Jiji.
Maelekezo yaliyotolewa kwa wafanyabiashara ndogondogo ni kutumia meza zenye maumbo yanayohamishika. Aidha Halmashauri ya Jiji haijazuia biashara ndogondogo kuendelea kufanyika katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa sasa vibanda vya kudumu vilivyojengwa kwenye maeneo hayo ya katikati ya Jiji vimekuwa kero kutokana na baadhi ya vibanda hivyo kujengwa mbele ya maduka ya wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuzuia wateja kuingia dukani aidha vibanda hivyo pia vimekuwa vikizuia njia za watembea kwa miguu hasa kwenye mabasi ya mwendokasi hivyo kuhatarisha usalama wao, pia vimekuwa vikizuia shughuli za usafi kutofanyika
Hivyo Mkurugenzi anasisitiza kwamba biashara katikati ya mji hazijazuiwa kama wengine walivyo tafasiri, muda umetolewa hadi mwishoni mwa mwezi Mei kwa wafanyabiashara waliojenga vibanda vya kudumu kuviondosha na kutumia maumbo yaliyoelekezwa.
Imetolewa na;
Tabu F. Shaibu
Mkuu wa kitengo cha Habari,Uhusiano na Mawasiliano
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Post a Comment