Sanlam ilivyokusudia kuwasaidia watanzania kupitia huduma ya Bima.
Taasisi ya kifedha isiyo ya kibenki Sanlam imejipanga kuhakikisha mteja wake wanaishi wakiwa na amani kutokana na huduma bora wanazotoa ambazo zinamtengenezea mazingira rafiki ili leo na kesho wawe na maisha bora.
Sanlam imetaja kuwa huduma za
bima zina umuhimu mkubwa kwa mstakabali wa taifa na kwa uchumi wa
wananchi .
Akizungumza na wanahabari mwisho wa wiki hii jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji Sanlam Julius Magabe, alisema kuwa kinga zitolewazo na kampuni ya bima , usaidia mlaji wa huduma kujikinga na athari za kiuchumi zitokanazo na majanga mbalimbali ikiwemo moto.
"Kwetu Sanlam tunajivunia kuwa sehemu ya utoaji wa kinga hii muhimu nchini Tanzania kupitia bima zetu mbalimbali zitolewazo na SGI & SLI , ulipa mafanikio ya bima yapatayo wastani wa Sh.40 billion kila mwaka," alisema Julius.
Julius alisema athari zingine zitokanazo na majanga mbalimbali ni pamoja na mafuriko, wizi, ajali, ulemavu na hata vifo, lakini pia usaidia kuweka akiba kwaajili ya mipango ya baadae.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kampuni yao mama imekuwepo kwenye biashara hiyo ya bima kwa muda wa miaka 103 mpaka sasa toka ianzishwe mwaka 1918 nchini Afrika Kusini.
Kampuni imejipambanua kuwa ndiyo taasisi ya kifedha isiyo ya kibenki inayoongoza kwa ukubwa barani Afrika ikiwa na biashara katika nchi 34 za Afrika.
Sanlam pia imekuwa na biashara katika mabara mbalimbali duniani ikiwemo bara la Asia, Marekani, Australia na Ulaya na inajivunia kwa uwepo wake katika nchin nyingi barani Afrika.
Tayari Sanlam imejiweka sehemu nzuri kihuduma kwani inakampuni mbili za bima kwa maana Sanlam General Insurance na Sanlam Life na Insurance.
"Kampuni zina uzoefu wa kulihudumia Soko la bima la nchini kwa miaka takribani 39 na hivyo inafanya hisia ya amani kwa kile ambacho ni cha muhimu kulindwa," alisema Julius.
Kwa upande wake Geofray Masige toka kampuni hiyo alisema uzoefu wao wa soko la bima nchini, ukijumlisha na uzoefu wa kimataifa inawafanya kuwa na uelewa mkubwa wa mahitaji ya soko na namna bora ya kuwafikisha huduma zinazokidhi mahitaji hayo.
Alisema Sanlam imebainisha kauli mbiu mpya ambayo inasema "Live With Confidence" ikiwa na maana Ishi kwa Kujiamini.
Wameeleza kuwa kauli hiyo inabeba ujumbe wa kufanya kila kitu kinawezekana kwenye utoaji wa huduma zao katika kumfanya mteja wao kuishi kwa kujiamini akiwa na amani kwa kuwa anayokinga madhubuti ya kifedha dhidi ya madhara yatokanayo na majanga mbalimbali.
Post a Comment