Ads

Ndege za kivita za Israel zafanya mashambulizi zaidi Gaza.

 

Picha zamtandasoni BBC

Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi mfululizo mapema leo katika maeneo kadhaa kwenye mji wa Gaza, saa chache tu baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuashiria kwamba vita vya nne dhidi ya kundi la Hamas vitaendelea. 

Miripuko mikubwa imeutikisa mji huo kutoka kusini hadi kaskazini kwa dakika 10 mfululizo, ikiwa ni mashambulizi makubwa zaidi kuliko yaliyowahi kufanywa kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Wawakilishi wa Norway, Tunisia na China katika wa Umoja wa Mataifa wameelezea masikitiko yao kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vifo vya raia na wametaka mashambulizi kusitishwa mara moja. 

Wapalestina 42 wameuawa kwenye mashambulizi hayo, ambayo Israel inasema yalilenga nyumba za makamanda wa Hamas.

Jumla ya Wapalestina 197 wameuawa tangu machafuko hayo yalipoanza Mei 10 na wengine 10 pia wameuawa ndani ya Israel.

Kutoka  DW

No comments