Mwlekeo mpya faini za barabarani
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la Polisi kutotumia makosa kama kitega uchumi kwa kutoza faini Madereva badala yake lijikite zaidi katika kutoa elimu.
Rais Samia Ameyasema hayo katika hafla ya Kuzindua Kiwanda cha Ushonaji sare za polisi kilichopo Bohari Kuu ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.
Aidha Rais Samia ameyataka majeshi mengine kuiga mfano wa jeshi hilo kwa kushona sare zao katika kiwanda hicho na kwamba hatua hiyo itadhibiti uingizwaji wa sare bandia mitaani na kuokoa fedha za serikali.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro, amesema takribani bilioni 50.1 zimekusanywa na polisi kutokana na makosa ya tozo za usalama barabarani kati ya Julai 2020 hadi Aprili 2021 wakati shilingi bilioni 56 zilizokusanywa kati ya Julai 2019 hadi Julai 2020.
Post a Comment