IGP Simon Sirro leo amemuapisha kamishina msaidizi wa Polisi ACP Salum Hamduni kuwa Kamishna
Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini Simon Sirro
leo amemuapisha kamishina msaidizi wa Polisi ACP Salum Hamduni kuwa Kamishna wa Polisi, jijini Dar es salaam.
kiapo hicho kimekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,
Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa
Kamishna na Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU.
IGP Sirro amempongeza kamishina HamdunI kwa weledi aliouonyesha katika
utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi hasa alipokuwa Kamanda wa Polisi katika
mikoa ya Ilala, Njombe, Kilimanjaro, Arusha na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum
Dar es salaam.
Kwa upande wake
Kamishina - SALUM HAMDUN
amemshukuru Mhe, Rais Samia Suruhu kwa kumuamini katika nafasi hiyo huku
akilishukuru Jeshi la Polisi kwa nafasi alizopata na kuzifanyia kazi kwa weledi
mkubwa.
Post a Comment