Ads

TANTRADE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHO YA 5 YA BIDHAA ZA VIWANDA VYANDANI

Naibu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka yamaendeleo ya  Biashara Tanzania (TANTRADE )  Bi Latifa  Mohamed Khamisi  akizungumza na waandishi wa habari ,hawapo Pichani (Picha  na John Luhende)

 Na John Luhende

Mamlaka yamaendeleo ya  Biashara Tanzania (TANTRADE ) ambayo ikochini ya wizara ya viwanda na Biashara  , imewataka watanzania kutembelea maonesho ya 5  ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayo tarajiwa kuanza tarehe 3 na kuendelea hadi  9  Disemba2020.

Akizunguza na waandishi wa habari  Naibu  Mkurugenzi  mkuu wa TANTRADE  Bi Latifa  Mohamed Khamisi   amesema,  maonesho hayo yanalengo la kuvitambua viwanda vya Tanzania na kuwahamasisha watanzania kupenda kununua na kutumia bidhaa zilizalishwa na viwanda vya Tanzania ambapo kauli mbivu ni "tumia bidhaa za Tanzania jenga Tanzania"

 "Tunatoa wito kwa watanzania  waje washiriki na kutazama maonesho haya kuona na kuzitambua bidhaa za tanzania  maonesho haya ni kitu kikubwa ambacho  kinawakutanisha wafanyabiashara mbalimbali  na wataweza kubadilishana uzoefu " Alisema 

Aidha amesema kutakuwepo na taasisi mbalimbali zinazosimamia  mnyororo waudhibiti wa biashara na viwanda  kama vile TBS, BRELA na zingine na utasaidia kutatua changamoto mbalilmbali . 

Katika maonesho hayo siku ya tarehe 6 kutakuwa na matembezi ya afya  joging itakayo anzia uwanja wa taifa na  program mbali mbali ikiwemo uhamasishaji wa unywaji maziwa ambapo watu wataonja maziwa kutoka viwanda vya Tanzania .

Pia kutakuwa na clinic ya Biashara ,wafanyabiashara wataeleza kila changamoto na wataalam watatoa   ushauri wa kibiashara  bure na hakutakuwa na kiingilio .

Pia kutakuwa na kongamano la biashara kupitia biashara  ambalo litafanyika tarehe 7 -8 na mwaka huu litahusha balozi za Tanzania nje ya nchi mabalozi watatoa maelezo mubashara akiwemo bolozi wa Kuwait ,Saudia Arabia ,Dubai, Abudhabi na link zote zitasambazwa  na mamlaka 

Pamoja na hayo Bi Ratifa amesema Mamlaka imewazingatia wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo na ghrama zimeshushwa ambapo kwa viwanda vikubwa watalipa 560,000 na viwanda vidogo  shilingi  100,000 hizo zote zina zinajumisha huduma zote watazopewa .

No comments