WAKULIMA TUMIENI MBOLEA ILI KUONGEZA UFANISI KATIKA KILIMO: DKT STEPHAN NGAILO
Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt.Stephan Ngailo akisisitiza jambo wakati wa kukagua ghala la kuhifadhia mbolea la SONAMCU mjini Songea
Pichani ni Mkaguzi wa Mbolea wa Mamlaka ya Udhibitibi wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw Allan Mariki akikagua moja ya maghala ya mbolea mkoani Mtwara.
Picha ikionesha shehena ya Mbolea iliyo hifadhiwa kwenye ghala la kuhifadhia mbolea la SONAMCU mjini Songea.
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo ametoa wito kwa wakulima nchini kutumia mboloea ili kuongeza ufanisi kwenye sekta ya kilimo.
Wito huo ameutoa alipo tembelea maghala ya mbolea kwenye Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe, kwa lengo lakujionea hali upatikanaji na usambaziji wa Mbolea nchini ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wakulima kwenye Mikoa yote inayo jishughulisha na kilomo cha mazao mbali mbali ya chakula na biasha.
Dkt Ngailo pia aliwataka maafisa kilimo kuhakikisha wanatoa elimu bora ya matumizi sahihi ya mbolea na kuhamasisha wakulima wanatumia mbolea hizo kwa kuwa hadi sasa mbolea ipo na itakidhi mahitaji ya wakulima nchini kote.
“Katika nchi nzima tuna zaidi ya asilimia 60 ya mahitaji yote ya mbolea, kufikia kati ya mwezi Februari hadi Machi tutakuwa na asilimia 75 hadi 80 ya mahitaji yote ya mbolea nchini hivyo ni wajibu sasa wa maafisa kilimo kuhakikisha wanatoa elimu na kuhamasisha wakulima kutumia mbolea iliyopo kwa usahihi ili kuongeza ufanisi kwenye sekta ya kilimo”. Aliongeza Dkt Ngailo.
Dkt.Ngailo amesema katika msimu huu, serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli imejipanga vizuri kuhakikisha wakulima wanapata mbolea za aina zote kwa wakati.
Hata hivyo amesema katika tathmini iliyofanyika Oktoba mwaka huu,Tanzania ilikuwa na tani zaidi ya 253,782, kati ya hizo tani 65,229 za mbolea ya urea na tani 35532 za mbolea ya kupandia (DAP) ambapo kiasi hicho cha mbolea kinaweza kufika hadi mwezi Februri 2021.
Akielezea hali ya kilimo Mkoani Ruvuma, Afisa Kilimo wa Mkoa huo Bw Paulo Msemwa amesema kuwa katika misimu miwili mfululizo ya 2018/2019 na 2019/2020 Mkoa umeongoza na kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula,huku sababu kubwa ya kuongeza uzalishaji ni upatikanaji na matumizi sahihi ya mbolea.
Bw Msemwa aliongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma unahitaji zaidi ya tani elfu hamsini (50,000) hadi sasa zimesha ingia tani elfu kumi na tatu (13,000)
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo anaendelea na ziara yake ya kukagua na kujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa Mbolea nchini kwenye Mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma na Tabora.
Post a Comment