Ads

TANCDA Inavyo pambania afya na uelewa mzuri kwa jamii katika magonjwa yasio ambukiza

Pichani anaye zungumza ni Dkt.Mashimbo mratibu kutoka NCD's mbele ya  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge Uratibu akipewa maelekezo juu ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza wakati wa  Kongamano la pili la Kisayansi la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo yaliyofanyika wiki moja sasa imepita Dar es Salaam

 Elimu ya kuelewa ugonjwa wa kisukari inaelezwa ,uelewa mzuri wa ugonjwa wa huo pamoja na dalili ni kiu ya mara kwa mara na unywaji wa maji mengi .

 Kutoona vizuri  au kupungua uwezo wa kuona,kukojoa mara kwa mara mkojo mwingi ,kizunguzungu pamoja na kupungua uzito  kusikoeleweka licha ya kula vizuri, pia dalili nyingine ni uchovu wa mwili bila kufanya kazi.

 Mtindo wa maisha ndiyo unaelezwa kuchangia sana uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari.

 Katika kijitabu kilicho tayarishwa na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa  Yasio ya Kuambukiza (TANZANIA NCD ALLIANCE  - TANCDA)na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari cha Tanzania (Tanzania Diabetes Association-(TDA) kimeeleza juu ya magonjwa hayo.

 Maana ya ugonjwa wa kisukari ni mlolongo wa matatizo mwilini,ya muda mfupi na mrefu,kutokana na upungufu au kutokomeza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa insulin

 Kichocheo hicho kimeelezwa kuwa kinaitajika ili mwili uweze kutumia sukari ipasavyo,kinatengenezwa mwilini na chembechembe za kiungo kinachoitwa kongosho.

 Sukari mwilini hutokana na chakula tunachokula na hutumika kuupa mwili nguvu :kufikiri , kupumua, moyo kupiga, kutembea, kumeng'enya chakula pamoja na kutengeneza kinga ya mwili.

 Pia sukari imeelezwa upigania , kupigana na vidudu vya maradhi wakati sukari ya ziada huwekwa akiba kwenye ini au huhifadhiwa mwilini kama mafuta.

Inaelezwa kuwa mtu akikaa muda mrefu bila kula , hifadhi hii hubadilishwa na ini kuwa tena sukari ili iweze kutumika.

 Magonjwa yasiyoyakumbukiza yamelisababishia Taifa hasara kubwa kwa kuondoa nguvu kazi na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya katika ufunguzi wa Kongamano la pili la Kisayansi la maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza wiki sssa imepita.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe alisema kwa takribani miaka nane magonjwa yasiyoyakuambukiza yamekuwa yakiongezeka ikiwa ni pamoja na gharama za matibabu.

Ameongeza kuwa lengo la Kongamano hilokuwa ilikuwa kuelewa kwa jamii kuhusu magonjwa hayo na njia za kukabiliana nayo ambapo katika wiki ya maadhimisho walitoa elimu kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari pamoja na kutoa huduma ya upimaji katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoyakuambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41 ambayo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016 huku mataifa ya Uchumi wa kati na chini kama Tanzania yakionekana kuathirika zaidi.

Dr. Mashombo Mkamba ambaye ni mratibu wa NCD's magonjwa yasiyo ya kuambukiza amesema kuwa kwa sasa kunaongezeko kubwa zaidi.

Anasema licha ya baadhi ya watu kuzoea pombe kama njia ya kujiburudisha inamadhara mengi kwa mnywaji.

"Watu wengi hupenda kunywa pombe vilabuni au nyumbani kwao kama njia ya kujistarehe, lakini pombe husababisha matatizo ya kiafya, yakiwemo magonjwa ya moyo, ini pamoja na majeraha yatokanayo na ajali zitokanazo na ulevi," anasema Dr. Mashombo.

Anasema wamekuwa wakifanya icha  kampeni kadha zinazopinga matumizi ya pombe, bado watu wengi wameendelea kushikilia kinywaji hiki bila kufahamu athari zake kwenye afya zao.

Meneja Mradi wa Shirikisho la Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA) Happy Nchimbi, amesema wamekuwa wakitoa upimaji wa afya kwa katika kampeni wanazozifanya juu ya ugonjwa wa kisukari

 Tatizo la ini.

Wataalamu ama matabibu wanasema unywaji wa pombe unaweza kusababisha maradhi ya ini yajulikanayo kama Cirrhosis; ambayo ni maradhi ya ini kushindwa kufanya kazi yake kutokana na uharibifu wa muda mrefu.

Shinikizo la Damu

Unywaji wa pombe kupita kiasi umethibitishwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maradhi ya shinikizo la damu.

 Imebainikia kuwa pombe huathiri mfumo wa usukumaji wa damu mwilini jambo ambalo hupelekea shinikizo la damu na baadaye matatizo mengine kama figo na ini kushindwa kufanya kazi.

Kupunguza Magonjwa yasiyo ambukiza inaelezwa kila mlo uwe na makundi yote matano ya vyakula ambayo ni (a)Nafaka ,Mizizi,Ndizi Mbichi za Kupika (b)Jamii ya Mikunde na Asili ya Wanyama (e)Mafuta.

Pia Ulaji wa vyakula halisi husaidia upatikanaji sawa wa sukari mwilini, kwa kuhifadhi na kumeng'enya pole pole chakula tumboni.

Jamii pia imeshauriwa kuwa sukari ikizidi mwilini huharibu mishipa ya damu nafahamu, macho ,figo na kongisho hivyo inashauriwa  kutoongeza sukari kwenye vyakula au vinywaji kwani sukari hiyo inapatikana mwilini haraka zaidi ya inavyotakiwa.

Jamii imetakiwa kupunguza unywaji wa pombe ama kuacha , inaelezwa kuwa pombe ni nishati ambayo haina virutubishi muhimu na badala yake huingilia uyeyushaji wa chakula na hufyonzaji na utumikaji wa virutubishi mbalimbali.

Unywaji wa Pombe unaelezwa kuwa unaweza pia kuchangia kwa kiasi kikubwa kusababisha madhara makubwa kwa mtumiaji na jamii na uharibifu wa Mali.

Na pia unaelezwa kuharibu ubongo,Ini,moyo na kongosho, magonjwa ya moyo ,kisukari.

Pamoja na magonjwa mengine kama saratani za kinywa ,koo, utumbo,matiti na tezi dume na uchochea utapiamlo na upungufu wa kinga ya mwili unaoweza kusababisha kifua kikuu.

No comments