Ads

Dkt. Mussa: Kufikia mwaka 2030 uelewa wa wananchi kuhusu masula ya bima uwe umefikia asilimia 80.

 
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt Mussa Juma akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Na Francis Peter

Mchango wa Sekta ya bima ukifikia asilimia 3 kwenye Pato la Taifa utakuwana matokeo chanya,hususan kwenye eneo la kuongeza thamani ya mazao ya kilimo,ufugaji,uvuvi na misitu hivyo mamlaka ya usimamizi wa bima nchini.

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt Mussa Juma ameitaka Menejimenti ya Mamlaka ya Bima (TIRA) na wafanyakazi wake kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa sekta ya bima inaongeza mchango wa pato la Taifa,kutoka asilimia 0.53 hadi kufikia asilimia 3 ifikapo mwaka 2030 kama mpango mkuu unavyotaka.

 Hayo yamezungumzwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa mamlaka hiyo ambapo amesema Mamlaka hiyo inatakiwa kufanya kila jitihada kuhakikisha mchango huo unafika asilimia 3 kufikia mwaka 2030.

“Mtakubaliana na mimi kwamba,sekta hii kuwa dumavu kunasababishwa na ushiriki mdogo wa watu au umma kwenye shughuli za bima,kwa sababu wengi wetu hatuna elimu ya kutosha ya masuala ya bima,nataka mpaka kufikia 2030 uelewa wa wananchi uwe umefikia asilimia 80 kwenye masuala ya bima”amesema Dkt. Mussa

 Amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA)imekuwa Katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia sekta, Mamlaka inafuata miongozo na  kanuni mbalimbali za utendaji kama inavyoelezwa na Serikali.

 Miongozo hiyo ni pamoja na Mpango Mkakati wa Miaka wa Mitano 2018/19 -2022/23 (CSP),Mpango kazi wa Mwaka Moja (Annual Action Plan) ambayo hutekelezwa na Mpango wa Bajeti (MTEF) ya kila mwaka wa fedha.

 Pia,Mamlaka imependekeza mabadiliko ya katika baadhi ya vipengele vya Sheriaya Bima 2009 na Kanuni zake ili kuendana na soko la bima kwa sasa.

 Amesema kwa kuzingatia miongozo hiyo,katika kipindi cha mwaka wa Biashara uliopita 2019 sekta ya bima iliandikisha tozo ghafi za bima kiasi cha shilingi Bilioni 813.761 na katika Mwaka 2020 yaani Januari Juni, sekta imeweza imeandikisha tozo ghafi za bima lenye thamani ya shilingi bilioni 433.336.

 Pamoja na tozo ghafi za bima kuongezeka kila Mwaka,Mamlaka bado mejiwekea malengo na mikakati ya kukuza soko la bima katika nyanja zifuatazo;kufikia wananchi wengi na huduma za bima (Insurancepenetration)kutoka asilimia 15 mpaka 50,kuongeza idadi ya mikataba ya bima inayokatwa kwa Mwaka (insurance uptake) asilimia 20 mpaka 60,na kuhakikisha wananchi wengi wanakuwa na uelewa wa huduma za bima kufikia 80% ifikapo Mwaka 2030.

 Katika kufikia malengo hayo,Mamlaka imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha yanafikiwa kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuruhusu njia mbadala za usambazaji wa huduma za bima kupitia mabenki,kuhuisha mfumo wa TIRA MIS ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato,kubadilisha mfumo wa ushughulikiaji majaladakutoka EDMS kwenda E-Office na kuhakikisha kuwa masuala ya kiuhasibu na fedha yanafuata mifumo ya kiserikali kwani kwa sasa

Mamlaka inatumia mfumo wa malipo wa MUSE tofauti na ule wa (SAGE) Vile vile, ili kuwa na takwimu sahihi, Mamlaka imeanza mchakato wa kuanzisha Kanzidata ya sekta ya bima ili kuwezesha Mamlaka kupata taarifa muhimu zitakazosaidia katika kupanga mikakati na kurahisisha ufanyaji wa maamuzi katika kuendeleza soko la bima.

Sambamba na hilo,Mamlaka ilitoa maelekezo kwa kampuni za bima zenye vituo vya kanzidata (Data Centers) nje ya nchi kuhakikisha vituo hivyo vinakuwa nchini na si nje ya nchi kama ilivyokuwa awali.

Pia,Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Bima kila robo Mwaka hujadili changamoto za soko na namna bora ya kuziondoa.

 Katika kipindi hiki, Ofisi ya Kamishna wa Bima imefanya vikao vya majadiliano na madalali wa bima; Wakaguzi bima na Wakadiria Hasara;Kampuni za bima; na Wamiliki wa hisa katika sekta ya bima.

 "Hatua hizi hazikosi changamoto mbalimbali ambazo kwa namna fulani huchangia sekta ya bima kutoendelea japo Mamlaka inajitahidi kupambana kukabiliana nazo;

 "Kutokuwepo kwa vipengele mbalimbali vya Sera na kisheria vinavyorahisisha usimamizi wa sekta ya Bima nchini hivyo kudumaza utendaji wa Mamlaka. Ili kutatua changamoto hii Mamlaka imeshaandaa Sera ya Taifa ya Bima (NIP) ambayo imewasilishwa Wizarani,"Dkt. Mussa.

Mamlaka inakabiliwa na upungufu wa fedha za kufanya miradi ya maendeleo kutokana na kutegemea makusanyo ya tozo za bima na adhabu zitokanazo na ukiukwaji wa taratibu za Biashara ya bima. Ufinyu huu umesababisha Mamlaka kutoajiri watumishi zaidi ili kuhakikisha sekta inasimamiwa vizuri.

 Mamlaka inaendelea kutengeneza mifumo ya TEHAMA itakayo saidia kudhibiti na kusimamizi wa mapato yatokanyo na huduma ya bima. Mpaka sasa watalamu hao wa TEHAMA wanaendelea na kazi. 

"Tunatarajia mifumo hii kuanza Januari 2021,mfumo huoutarahisisha ukusanyaji mapato, kuwa na stika za magari za kielektroniki,ukusanyaji taarifa na usimamizi kwa ujumla na kurahisisha upatikanikaji wa takwimu na taarifa,"amesema Dkt. Mussa.

 

Aidha anasema  TIRA itaendelea kupokea na kufanyia kazi maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Serikali ili kuendana na kasi ya kukuza uchumi kama inavyolinatiliwa mkazo na Mheshimiwa Rais.

 

Pia,katika kuhakikisha soko la Bima linakuwa kwa kasi halisi,Mamlaka inafanya tafiti mbalimbali na kukusanya taarifa ili zisaidie kuweka mikakati thabiti kulingana na changamoto zilizobainishwa na tafiti

hizo. 

"tunasimamia kwa karibu kampuni za bima ili kuhakikisha

changamoto ya ukwasi na mitaji zinakabiliwa mapema kabla

hazijaathiri mfumo wa mzima wa sekta ya Fedha,"Anasema Dkt.

Mussa.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi idara mipango kutoka Wizara ya Fedha

na Mipango Theresia Henjewele ameitaka kujadili kwa pamoja katika

vikao vyao na kufanya mipango ya kuyafukia malengo yao ndani

ya miaka 10 ili kufikia asilimia 3 ya uchangiaji katika pato la

Taifa.

No comments