SERIKALI YAENDELEA KUTOA ELIMU DHIDI YA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Licha ya Jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na Wadau wa afya katika kusaidia kutokomeza Magonjwa yasiyoambukiza lakini bado Takwimu Nchini zinaonyesha magonjwa yanaendelea kuongezeka ambapo kati ya vifo 134,600, asilimia 33 ya vifo vyote hutokana na magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza Jana Jijini Dar es salaam Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abeli Makubi Katika Ufunguzi wa Kongamano
la pili la kisayansi la Maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza ambapo kutakuwepo na utoaji wa elimu,upimaji,juu yamagonjwa hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
Profesa Makubi alisema Takwimu za Shirika la Afya Dunian(WHO)zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoambiza yanachangia vifo zaidi ya milion 41 ambapo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milion 57 vilivyotokea mwaka 2016 hali hiyo husababisha mataifa ya Uchumi wa kati kama Tanzania kuathirika .
"Kwa mujibu wa Takwimu ya Shirika la Afya duniani magonjwa yasiyoambukiza yanachangia vifo zaidi ya Milioni 41 ambapo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote million 57 ambayo husababisha uporomokaji kiuchumi" Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee, na Watoto Dkt Grace Magembe alisema Kwa miaka iliyopita Magonjwa yasiyoambukiza yalikuwa yanasumbua zaidi lakini kwa zaidi ya miaka nane sasa Magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakiongezeka na kusababisha serikali kutumia gharama kubwa na kuyapatia ufumbuzi.
" Kwa zaidi ya miaka nane sasa Serikali imekuwa ikijikita zaidi katika kuhahakikisha wananchi wanapata huduma ya afya kwa upende wa magojwa yasiyoambukiza Serikali imekuwa ikitoa gharama kubwa kutoa huduma" Alisema.
Nae Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) profesa Andrew Pembe alisema chuo kitaendelea kufanya tafiti mbalimbali na kutoa miongozo na kutoa njia za kutatua matizo ya Afya hususani magonjwa yasiyoambukiza.
"Chuo Kikuu Cha Sayansi na Shirikishi Muhimbili kinaendelea kutoa miongozo sahihi kusaidia kutoa njia nzuri itakayosaidia kutatua changamoto ya magonjwa yasiyoambukiza". Alisema.
Post a Comment