RAIS WA ZANZIBAR DK MWINYI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI
………………………………………………………………….
Zanzibar
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amesema hakuunda serikali serikali ya umoja wa kitaifa (suk)kwakuwa hadi sasa chama cha Act wazalendo bado wawakilishi wa chama hicho hakijawasilisha majina ya wajumbe wake wa baraza la wawakilishi na kula kiapo .
Amesema msimamo wake bado uko pale pale wa kuundeleza maridhiano na kuendeleza umoja miongoni mwa wazanzibari kwa mujibu wa katiba ya zanzibar ya mwaka 1984.
Akizungumza leo ikulu jijini zanzibar Rais Dk alisema yuko tayari kukutana naye wakati wowote na kuwashirikisha kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ikiwemo kuteua na kulitangaza jina la Makamo wa Kwanza wa Rais.
Alisema kwa mujibu wa katiba ofisi ya Rais imeshapeleka barua katika chama cha Act Wazakendo na kuwataka kutuma majina ya wawakikishi wao lakini hadi leo bado hawajafanya hivyo.
Rais huyo alisema kwakuwa muda bado ungalipo anaamini wenzao wa upinzani ambao wamepata zaidi ya asilimia kumi watatimiza wajibu wao na kuwasilisha majina ya wawakilishi wao na jina likiwemo jina la makamo wa kwanza wa Rais.
Aidha Rais huyo wa zanzibar alisema kama alivyoahidi wakati wa kampeni kuhusu sekta ya michezo atahakikisha anashirikiana na vyama na wadau wa michezo katika azma ya kukuza michezo yote katika utawala wake.
Dk Mwinyi ametamgaza baraza hilo jipya la yajayo ni neema tupu likiwa na wizara kumi na tano halina manaibu waziri kwa wakati huu hadi hapo baadae .
Dk Mwinyi alisema katika baraza hilo ameuziunganisha baadhi ya wizara kwa mintaraf ya kukuza utendaji na ufanisi wenye tija ,viwango na manufaa kwa maendeleo ya nchi na wananchi kulingana na matakwa ya katiba na sera.
Mawqziri na wizara zilizoundwa na mawaziri husika ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji itaongozwa na Mudrik Ramadhan Soraga.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Masoud Ali Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman.
Aidha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi – Dkt Khalid Mohammed Salum,Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo Soud Nahoda Hassan.
Wizara nyingine ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali itaongozwa na Simai Mohammed Said wakati Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni Tabia Mwita Maulid, Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri huku Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Riziki Pembe Juma.
Hata hivyo Rais Dkt Mwinyi anetangaza Wizara ya Maji na Nishati ameteuliwa Suleiman Masoud Makame, Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Haijapata Waziri wakati Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale aneteuliwa Lela Mohammed Mussa, Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi Abdallah Hussein Kombo ambapo Wizara ya Ujenzi imeshikwa na Rahma Kassim Ali.
Post a Comment