MANISPAA YA ILALA YAWATUNUKU VYETI WAFANYA BIASHA VINARA WA KULIPA KODI.
Mmoja wa wafanyabiashara akikabidhiwa cheti na mkuu wa wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija aliye upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Ilala Christopher Myava , akikabidhiwa cheti kwaniaba ya TAKUKURU mkoa wa Ilala ,hapo akipngezwa na mweka hazina wa manispaa ya Ilala Turusubya Kamaramo
Baadhi ya wafanya biashara walio hudhuria hafla ya kutunukuvyeti wakisikiliza hotuba ya DC Ludigija (Picha zote na John Luhende )
Na John Luhende
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imesema , inampango wa kuanzisha kituo kikubwa cha pamoja cha mlipa kodi ( One stop center) kwaajili ya kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara na kuongeza makusanyo ya kodi.
Pia kimeanzishwa kituo cha walipa kodi Buguruni ,kunampango wa kuanzisha nyingine maeneo ya Tabata na Kinyerezi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija wakati wa hafla ya kutunuku vyeti kwa wafanya biashara wa Manispaa hiyo kwa kutambua mchango wao Katika kusaidia kukusanya kodi.
Manispaa hiyo mwakajana ilikusanya shilingi Bilion 58 na kuvuka lengo la kukusanya bilioni 57.
Amesema Dar es salaam kwa mwaka huu imetumia zaidi ya shilingi bilioni 660 Katika ujenzi wa miundombinu ambapo fedha hizo ni za walipa kodi.
Ameongeza kuwa , Manispaa itaendelea kuwainua akinama na vijana na walemavu kupitia mfuko wa Manispaa unaotoa asilimia 10 ya mapato.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumane Shauri amesema kuwa, mwaka 2019 walitarajia kukusanya shi bill 57 lakini kutokana elimu inayotolewa na Manispaa hiyo wamevuka malengo na kukusanya sh Bill 58 sawa na asilimia 103.
Amesema kuwa, kutolewa kwa vyeti hivyo kwa wafanyabiashara vitakua chachu ya kuleta Maendeleo na uzalendo kwa wananchi kwani Maendeleo ya nchi hiyo yataletwa na wafanyabiasha wote.
Naye, Mweka Hazina wa Halmashaur hiyo,Turusubya Kamaramo, amesema kuwa,Manispaa ya Ilala kwa miaka 3 kutoka 2017/19 imevuka malengo ya kukusanya Kodi kutoka Sh Bill 46 hadi kufikia sh Bill 58 sawa na asilimia 10 , mwaka 2020/21 wanatarajia kukusanya sh Bill 60.
Mwakahazina huyo amsema ,wanatarajia kuandaa mpango kazi kwa mapungufu yote walioyagundua kutoka kwa wafanyabiashara ili kuweza kufikia malengo ya kukusanya sh Bill 100 kwa mwaka 2020/25 na kutoa hamasa kwa wafanyabiashara wengine waweze kulipa kodi.
Kwa upande wakeKamanda wa TAKUKURU mkoa wa Ilala Christopher Myava , amewataka wafanya biashara kulipa Kodi na kutoa risti halali ili kuepuka udanganyifu na kukwepa kulipa kodi na kusema kuwa taasisi hiyo haita sita kuchukua hatua kwa wakwepa kodi.
"Kunabaadhi ya watu ambao wanatakiwa walipe kodi lakini hawalipi kodi haya mapato ya haya ya bilioni 58 bado ni machache kunapesa nyigi bado zipo nje sisi kama taasisi huwa tunafanya tafiti zinazoisaidia Serikali kukusanya mapato"alisema Myava.
Taasisi inaendela na uchunguzi kuna baadhi ya wafanya biashara wajanja wajanja wanatumia mashine za kukusamapato kuweza kujinufaisha ,wanatoa risiti lakini si halali ,wengine wanauza risiti zisizo halali fedha haziingii katika mamlaka ya mapato ,kilammoja akishiriki kikamilifu taifahili litasonga mbele.




Post a Comment