JAMII FORUMS NA CDF ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KIKAZI ,KUTOA ELIMU ,KUPINGA UKATILI
Mkurugenzi mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti aliye upande wa kushoto na aliye upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Jamii forums Maxence Melo wakionesha mkataba wa makubaliano ya ushirikiano walio usaini baina ya taasisi zao leo jijini Dar es salaam.( Picha na John Luhende)
Mkurugenzi mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti aliye katkati na aliye upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Jamii forums Maxence Melo wakisain mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi zao leo jijini Dar es salaam.( Picha na John Luhende)
Na John Luhende
Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) na. asasi ya kiraia ya Jamii Forums ambayo inaratibu mtandao maarufu nchini wa Jamii Forums leo wamezindua ushirikiano wa kikazi.
Akizungumza Katika uzinduzi huo Mkurugenzi mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti , amesema ushirikiano huo unalengo la kukuza uelewa wa haki na ustawi wa Mtoto wa kitanzania Katika harakati za kutokomeza ukatili dhidi ya Watoto ikiwemo mimba za utotoni , ukeketaji, ndoa za utotoni,ubakaji na ulawiti ,vipigo, matusi matusi na udhalilishaji wa utu wa mtoto.
Amesema Katika ushirikiano huo utawezesha kutoa elimu kupitia mtandao wa Jamii Forums ambao unaongoza kwa kusomwa na watu wengi ndani na nje ya nchi ukiwa na wasomamaji takribani Milioni kumi Kila mwezi jambo ambalo litawezesha kutoa elimu kwa jamii juu ya Sheria na Sera zinazo mlinda mtoto wa kitanzania, mila na tamaduni zinazo zinazomkandamiza mtoto, wajibu wajamii kwa mtoto .
Aidha elimu itatolewa juu ya namna ya kuripoti kesi za ukatili katika vituo husika moja wapo ikiwa no katika dawati la jinsia na watoto, vituo vya mkono kwa mkono ili kuwezesha kupatikana kwa haki.
Ushirikiano pia utasaidia kupaza sauti na kutoa elimu kwa jamii na wahanga wa matukio ya ukatili kujua haki zao na kuendeleza juhudi zinazo fanywa na Serikali, Asasi za kiraia , wadau wa maendeleo, Vyombo vya habari.
Kwamujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi yakuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU umeonesha kuwa asilimia 84.5% ya vitendo vya rushwa ya ngono hufanyiwa wanawake na asilimia 15.4 hufanyiwa wanaume .
Utafiti mwingine wa Demographia na Afya TDHS za mwaka 2015/2016 unaonesha asilimia 36 ya wanawake nchini Tanzania wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2019 iliyo tolewa na kituo Cha Sheria na haki za Binadamu ilibainisha asilimia 84 ya matukio ya ukatili dhidi ya Watoto yaliripotiwa na vyombo vya habari mwaka 2019 ni ya ukatili wa kingono, pia matukio 42,824 ya ukatili wa kijinsia dhidi ya Watoto yaliripotiwa Polisi mwaka 2016-2019 yalikuwa ya ukatili wa kimwili,kingono, utumikishwaji kazi,ubaguzi kwa wanaoishi na ulemavu.
Utafiti mwingine wakidemographia na Afya TDHS wa mwaka 2015-2016 unaonesha asilimia 27%ya wasichana Kati ya miaka 19 walipata ujauzito .
Kwa mwaka 2003 -2011 wanafunzi 55,000 waliacha shule kwa sababu ya mimba za utotoni wengi wakiwa kati ya miaka 13 hadi 18.


Post a Comment