DKT.TULIA ACHAGULIWA KUWA NAIBU SPIKA
Naibu Spika wa bunge la 12 Mhe.Dkt.Tulia Ackson kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) akiwashukuru wabunge waliomchagua kwa kishindo wakati wa Bunge la 12 Jijini Dodoma leo tarehe 12 Novemba 2020.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mhe.Dkt. Tulia Ackson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12.
Dkt. Tulia ameshinda kwa kishindo baada ya kupata kura 350 ambapo wapiga kura walikuwa 354 Dkt.Tulia amepata kura 350
Uchaguzi huo umefanyika leo tarehe 12 Novemba 2020, jijini Dodoma ambao ulitanguliwa na uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Akiomba kura kwa wabunge Mhe. Dkt. Ackson amesema kuwa atajitahidi kuwatumikia wabunge wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha amesema kuwa atamshauri vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumia uzoefu alionao ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.
Akitoa neno la shukurani mara baada ya kuchaguliwa Mhe. Dkt. Ackson amewashukuru wabunge wote kwa kumchagua kwa kura za kishindo atafanya kazi bega kwa bega na wabunge wote.
“Naahidi nitawatumikia kama mtumishi wenu, tutafanya kazi kiufanisi na pia nitatumia weledi wangu katika kazi zangu kama Naibu Spika, naomba msisite kuniletea hoja zenu pale mnapokuwa nazo” amesema Mhe. Dkt . Ackson
Post a Comment