Serikali, Wazalishaji Saruji waweka mambo sawa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -
Uwekezaji, Mh. Angellah Kairuki pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh.
Innocent Bashungwa wakijadili masuala mbalimbali na wazalishaji wa saruji
nchini kwa lengo la kujadili fursa, changamoto na namna bora ya kukuza sekta ya
ujenzi nchini kupitia saruji, kikao kilichofanyika Ofisi za Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC), jijini Dar es Salaam.
..................................
Imeelezwa kuwa Sekta ya Ujenzi ni miongoni mwa sekta zinazokua kwa kasi nchini, hii ni kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Kairuki alisema kuwa wizara yake na Wizara ya Viwanda wanafanya kazi kwa ukaribu na kuwatoa hofu wazalishaji hao wa saruji kuwa serikali ipo pamoja nao na inashughulikia changamoto zao na kuwahakikishia wizara yake yenye dhamana ya uwekezaji itahakikisha inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hao.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa aliwahakikishia wazalishaji hao kuwa serikali ina angalia namna bora ya kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi hasa kwa viwanda vilivyopo Ukanda wa Pwani pia amewahakikishia kuwa changamoto nyingine ndogo ndogo atazishughulikia ndani ya wiki moja ijayo.
Post a Comment