BREAKING NEWS JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM, LABAINI MBINU CHAFU ZA KUHATARISHA AMANI
Na John Luhende KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Lazzaro Mambosasa, amesema jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vya watu wanaofanya mikutano ya siri ili kuhamasisha vurugu na maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Amesema jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha halitoi nafasi ya kufanyika kwa vurugu ili kuheshimisha Demokrasia nchini na maamuzi ya wananchi. Amevitahadharisha vikundi hivyo viache mara moja mipango hiyo kwani vitakutana na adha kubwa ya Vyombo vya Dola. Kadhalika Mambosasa, ameongeza kwa kuwataka wananchi watoe taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pindi wanapobaini ama kuhisi uwepo wa watu wanaohamasisha vurugu ili kudhibiti hilo mapema.
|
Post a Comment